Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa (MB), amesaini kitabu cha wageni na kukabidhiwa Taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za maendeleo za Mkoa wa Arusha na Mhe. John V.K Mongella muda mfupi kabla ya kuzungumza na watumishi na viongozi wa mikoa hiyo miwili.
Hata hivyo, Mhe. Mongella amekabidhi taarifa ambayo imesheheni mafanikio makubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kisekta, inayokadiriwa kugharimu takribani shiligi trilioni 3, miradi ambayo licha ya ubora wake, imefanya mapinduzi makubwa katika utoaji na upatikanaji wa huduma za kijamii katika mkoa wa Arusha, huduma ambazo zikiwa zimesogezwa karibu na wananchi.
"Mkoa wa Arusha, naweza kusema ni mkoa uliopendelewa, kwa kupata miradi mingi ya maendeleo katika sekta za elimu, afya, maji, miundombinu ya barabara na umeme, sekta ya Utalii pamoja na filamu ya Royal Tour, iliyoleta mapinduzi katika pato la wakazi wa Arusha, linalochangia uchumi wa mkoa na Taifa kwa ujumla, Arusha ya sasa sio ya zamani, viongozi na wananchi wanashirikiana katika kuleta maendeleo" Ameweka wazi Mhe. Mongella.
Aidha, Mhe. Mchengerwa, amekabidhi magari 13 yaliyotolewa na Serikali kwa ajili ya Usimamizi Shirikishi wa Shughuli za Afya kwenye mikoa ya Arusha na Manyara, huku mkoa wa Arusha ukupata magari 5 na Manyara magari 8, shughuli iliyofanyika leo tarehe 13.12.2023 kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.