Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K.Mongella ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la wavulana shule ya sekondari Kitumbeine wilaya ya Longido mradi unaotekelzwa na Serikali kupita Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) OPEC IV katika kijiji cha Lopolosek.
Akisoma taarifa ya mradi huo, Katibu wa Mradi wa Jamii Kijiji cha Lopolosek, Isaya Kalanga amesema kuwa mradi huo wa bweni la wavulana, unategemea kutumia shilingi milioni 155.8, bweni ambalo linategemea kulaza jumla ya wanafunzi 80.
Amesema shule hiyo inawanafunzi zaidi ya mia nane hiyo mradi huo ni muhimu shuleni hapo kwa kuwa utapunguza msongamano wa wanafunzi uliopo kwenye mabweni yaliyopo sasa.
Aidha kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho hakusita kuishukuru serikali ya awamu ya sita na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali watoto wa wafugaji, ili nao wapate elimu kwenye mzazingira bora kama ilivyo kwa watoto wengine wakitanzania.
#ARUSHAFURSALUKUKI
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.