Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Bweni la wavulana shule ya sekondari Kitumbeine kijiji cha Lopolosek wilaya ya Longedo leo tarehe 22 Desemba, 2023.
Mhe. Mongella ameagiza wakuu wa shule, kusimamia utunzaji wa miundo mbinu ya shule ikiwemo majengo, vifaa vya shule, wanagunzi pamoja na walimu.
Ametoa rai hiyo mara baadanya kujionea uharibifu wa majengo ikiwemo kuta kuchafuka na baadhi ya madirisha vioo vyake kuvunjika na kusisitiza kuwa, mkuu wa shule anaowajibu wa kusimamia utunzani wa vifaa vya shule pamoja na kufanya ukarabati mdogo pale unapotokea uharibifu na sio kusubiri serikali kufanya hayo.
"Mwalimu mkuu, ni mkuu wa Taasisi mali na watumishi, endapo atashindwa kusimamia majukumu yake inamaanisha hatoshi, niwaagize wakuu wa shule wote, kusimamia utunzaji wa mali za shule, kazi ya mkuu wa shule ni kusimamia taaluma pamoja na vitendea kazi vyote vinavyosaidia taaluma kusimama imara"
Ameongeza kuwa, yapo mafungu ya uendeshaji wa shule, ambayo ipo asilimia ya ukarabati na kuwataka walimu kutumia fedha hizo kukarabati uharibifu mdogo mdogo unaojitokeza na sio kuacha mpaka majengo yachakae.
"Serikali inawekeza fedha nyingi kujenga majengo ya shule, ni jukumu la walimu kuwasimamia wanafunzi kuyatunza, hakuna maana ya kujenga baada ya miaka mitatu jengo halifai, Walimu kuweni wazalemdo, tunzeni miundombinu yote ya shule" Amesisitiza Mhe. Mongella
Awali, mradi huo wa bweni la wavulana, shule ya sekondari Kitumbeine umegharimu shilingi milioni 155.4 fedha kutoka Serikali Kuu, kupitia mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, OPEC awamu ya IV.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.