Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, ametembele na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa shule mpya sekondari ya Wasichana Orbomba, wilaya ya Longido.
Mhe. Mongella licha ya kukiri ujenzi wa mradi huo kuendelea vizuri, amewataka watalamu kuongeza kasi ya ujenzi, ili mradi ukamilike kwa wakati, na wanafunzi kuanza masomo mapema Januari 2023.
Ameshauri, wakandarasi kuongeza idadi ya mafundi wa wa kujenga pamoja nakugawa kazi tenda ya kutengeneza milango na madirisha kwa mafundi tofauti ili kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.
"Adhma ya Rais wetu mama Samia ni wanafunzi kuanza shule wka wakati, mapema Januari, fanyeni kazi usiku na mchana, kwa kazi hii, sikuu ifanyike hapa, ili tusipoteze muda, kwa kuwa tuko nyuma ya muda" Amesema Mhe. Mongella
Mradi huo, unatekelezwa kwa fedha kutoka Serikali kuu shilingi Bilioni 3 kupitia mpango wa kuboresha elimu ya Sekondari nchini.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.