RC MONGELLA AKIWASILISHA TAARIFA YA MAANDALIZI YA MAPOKEZI YA WANAFUNZI JANUARI 2024 KWA WAZIRI TAMISEMI KUPITI ZOOM.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, amewasilisha taarifa ya mkoa huo, ya Maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa darasa la awali, la kwanza na kidato cha kwanza, mwaka wa masomo unaotarajia kuanza mapema Januari 2024, wakati wa Kikao kazi cha wakuu wa Mikoa na Waziri Ofisi ya Raisi TAMISEMI Mhe. Mchengerwa kupitia mkutano wa Zoom leo tarehe 30 Desemba, 2023.
Akiwasilisha tarifa hiyo, Mhe. Mongella amesema kuwa, mkoa wa Arusha umejiandaa vema kupokea wanafunzi wanaoanza shule, mwaka wa masomo unaoanza Januari 2024, kutokana na ukweli kuwa, Serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kuboresha miundombinu yote muhimu kwa shule za msingi na sekondari.
Amefafanua kuwa, hali ya uandikishwaji wanafunzi wa darasa la awali imefikia asilimia 56, wakiwa tayari wameandikishwa watoto 39,054 kutoka maoteo ya watoto 69,174, darasa la kwanza wakiandikiswa watoto 46,002 kutoka maoteo ya watoto 62,307 sawa na asilimia 74, huku wanafunzi 180 wakiwa wameandikishwa kwenye madarasa ya MEMKWA.
Amebainisha kuwa, mpaka kufikia tarehe iliyopangwa na Serikali, shule kufunguliwa tarehe 08 Januari, 2024, mkoa wa Arusha unatarajia hali ya uandikishwaji itakuwa imeongezeka na kufikia asilima 100 na hatimaye kufikia malengo ya kuandikisha wanafunzi kwa mkoa, kulingana ya idadi ya watoto wenye umri wa kuanza masomo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.