• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

RC MONGELLA AKIZUNGUMZA NA BALOZI WA VIETNAM NCHINI TANZANIA

Posted on: July 26th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mhe.John V.K Mongella leo tarehe 26/07/2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Vietnam Nchini Tanzania Mhe. Nguyen Nam Tien.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Balozi Nguyen amelezea uhusiano mkubwa wa Kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Vietnam kuwa umedumu tangu mwaka 1965 mara baada ya Muungano wa Serikali ya Tanganyika na Zanzibar kuungana,huku akitabaibisha  kuwa uhusiano huo ulijengwa zaidi ya Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere chini ya mfumo wa Siasa za Kijamaa.

Aidha,Balozi Nguyen aliendelea kueleza kuwa Vietnam imefurahishwa na Uongozi wa Rais Dkt Samia kwa kusimamia kwa dhati Siasa za Kiplomasia za Kiuchumi kwa kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na Mazingira mazuri na tulivu ya kiuwekezaji na kuhahidi kutumia fursa hiyo katika kuwaleta wawekezaji na wafanyabishara toka Vietnam kuja Arusha kwaajili ya kuangalia fursa mbalimbali zilipo.

Balozi Nguyen amesema kuwa Vietnam ni Nchi ya 40 katika ukuaji wa Kiuchumi Duniani na  amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mhe.John Mongella kuwa  Vietnam iko tayari kushirikiana Tanzania hususan Arusha katika kubadilishana utaalam  mbalimbali ikiwemo maendeleo Viwanda  na Teknolojia ya Mawasiliano kwani tayari Vietnam wanaendesha makampuni ya Mawasiliano ikiwemo Kampuni ya Simu ya HALOTEL.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella amemweleza Balozi Nguyen kuwa Arusha ina fursa rukuki zikiwemo Utalii,Kilimo,Mifugo na Viwanda hivyo kumwomba kuitangaza Arusha Nchini Vietnam kwa kuwaalika Wawekezaji toka Sekta mbalimbali kuja kuwekeza katika Mkoa wa Arusha kwani Mkoa Una mazingira mazuri ya kiuwekezaji na miundombinu inayorahisha shughuli za uwekezaji ikiwemo Viwanja vya ndege vya KIA,Reli ya Arusha kwenda Dar na barabara za uhakika zinazopitika majira yote ya Mwaka.

Aidha,Mhe.Mongella amemweleza Balozi kuwa Serikali ya Rais Dkt.Samia imeweka kipaumbele Kikubwa katika kuweka mazingira wezeshi kwa Wawekezaji kuja kuwekeza Nchi Tanzania hii imetokana na kusimamia vyema Sera ya Diplomasia ya Kiuchumi ambayo mpaka sasa Tanzania inaendelea kunufaika na Sera hiyo Duniani.

Vile vile Mongella amesema Arusha ni lango Kuu la Utalii kwani asilimia kubwa ya Watalii wanaingia Tanzania hupitia Arusha  hivyo kutoa fursa kubwa kwa Wawekezaji toka Vietnam kuja kuwekeza katika Sekta ya Utalii kwa kuendesha biashara ya  Hotel pamoja na Usafirishaji Watalii.


Balozi wa Vietnam Nchini Tanzania yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi

Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.