Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John V.K Mongella, amekutana na kusalimiana na wageni kutoka Marekani, wakiongozwa na Sesly Thomas, wakiwa Wilaya ya Longido kwa ajili ya kutembelea miradi wanayoifadhili katika hiyo.
Wageni hao wametembelea na kufutilia miradi wanayoifadhili, ikiwa ni pamoja na mradi wa kutoa lishe kwenye shule za Mundarara na Emuroto, mradi ambao utawezesha kupata chakula katika shule hizo.
Kama inavyofahamika kwa uliopita wa mwaka 2023, wananchi wa wilaya ya Longido walikumnwa na baa la njaa, kufuatia changamoto hiyo, licha ya kutoa chakula shuleni kwa wadau hao wa shirika la Convoy of Hope, walifanikiwa pia kutoa chakula kwa kaya 1,200, na shirika linatekeleza Miradi mbalimbali utoaji wa huduma za Maji na Mifugo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.