Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella ameahidi kwa niaba ya wakuu wa mikoa yote Tanzania kuongeza kasi katika kutekeleza Mkataba wa Afua za Lishe nchini kama yalivyo maelekezo ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa na SSerikali
Mhe. Mongella ameahidi hayo mbele ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wakati wa Mkutano wa tisa wa Wadau wa Lishe nchini, uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mkoani ArArusha
Amesema kuwa Afua za Lishe ni ajenga muhimu yenye lengo la kuboresha hali ya lishe na kupunguza athari za utapiamlo na udumavu kwa watwato
"Mhe. waziri Mkuu nikuahidi kwa niaba ya wakuu wa mikoa wenzangu, tutaendelea kuwajibika na kutekeleza majukumu yetu na kuchukua hatua madhubuti za kupunguza hali duni ya lishe katika mikoa yetu kwa kuzingatia zaidi maelekezo ya ofisi yako, Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Rais TAMITAMISEMI
Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa, ameweka wazi kuwa mkoa wa Arusha ni kati ya mikoa, inayofanyia kazi kwa mikataba ya Lishe, katika ngazi zote na kupata mafanikio makubwa ambayo yamepatikana chini ya viongozi wetu wakuu wa nchinnchi
Awali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama (MB), amesema kuwa Mkutano wa tisa wa Wadau wa Lishe umefanyika mkoani Arusha kwa sababu mkoa huo unafanya vizuri katika utekelezaji wa afua za Lishe nchininch
Mkataba wa Lishe ni mkakati wa Kitaifa ambao ulisainiwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma mwaka 2022 na baadaye kusainiwa na Wakuu wa mikoa, wakurugenzi wa hamashauri kupitia ofisi ya Mkuu wa mkoa na hatimaye Maafisa Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji Tanzania nzima.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.