Na Daniel Gitaro
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella amewataka wananchi wa mkoa huo, kujitokeza katika zoezi la Kitaifa la Kuchangia Damu Salama, na kujitolea damu ili kuokoa maisha ya watu wanaohitajia damu kwa dharura.
Mhe. Mongella ametoa wito huo wakati wa uzinduzi wa zoezi la Uchangiaji Damu Kitaifa liliandaliwa na Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na kuwakutanisha wadau kutoka madhehebu yote nchini, zoezi liliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Arusha.
Amesema kuwa, zoezi hilo linalenga kukusanya damu Salama na ili kuwa na akiba ya damu kwenye hospitali zetu, damu ambayo itatumika kwa wagonjwa wenye uhitaji, hususani wagonjwa wa dharura waliopata ajali na kuokoa maisha, ikiwa ni kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya maridhiano inayotarajiwa kufanyika Machi 6, 2024.
Kujitolea damu ni tendo la thawabu kubwa kwa Mungu, kwa kuwa damu ni zao pekee ambalo haliwezi kununuliwa kwa thamani yoyote ya fedha, bali kwa kujitolea kwa wananchi wenyewe.
“Ninawaomba wanaarusha tujitokeze kwa wingi kuchangi damu,kwa kuwa kuna uhitaji mkubwa sana wa damu salama, Damu ni uhai hivyo unapotoa sehemu ya uhai wako na kuokoa wengine unapata thawabu kutoka kwa Mwenyenzi Mungu"
Hata hivyo, amethibitisha kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea na mkakati wa kuboresha miundombinu ya sekta ya afya na vifaa tiba, lakini yote hayo yatakuwa na manufaa zaidi ikiwa wananchi watajitoa kwa wingi kuchangia Damu Salama.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Sheikh, Dkt. Alhad Mussa Salim, licha ya kuendelea kusisitiza wananchi kushiriki katika zoezi hilo, ameipongeza Serikali ya Awamu ya sita kwa kuendelea kudumisha amani nchini, katika masuala ya kidini na kisiasa jambo ambalo linaleta umoja kwa wananchi wake.
“Sisi tunafanya maridhiano na amani katika nchi yetu, lakini wananchi hawawezi kuwa na amani kama wanasumbuliwa na maradhi na zoezi hili la kuchangia damu halibagui dini wala imani yoyote bali hii ni kama sadaka na ibada yenye maana Zaidi.”
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Taifa, Askofu Israel Maasa amemshukuru sana Mkuu huyo wa Mkoa kama mlezi wa Jumuiya hiyo Mkoani hapo kwa ushirikiano mkubwa anaoonyesha katika kuleta maridhiano ka kuhakikisha kuwa Amani inadumu.
Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea na mkakati wa kuboresha miundombinu ya sekta ya afya, ununuzi wa vifaa na vifaa tiba hasa katika mkoa wa Arusha lakini yote hayo yatakuwa na manufaa Zaidi ikiwa wananchi watajitolea michango yao ikiwemo kuchangia damu salama kwa wahitaji.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Sheikh, Dkt. Alhad Mussa Salim, licha ya kuendelea kusisitiza wananchi kushiriki katika zoezi hilo la Kitaifa ameipongeza Serikali ya Awamu ya sita kwa kuendelea kudumisha Amani katika Nchi yetu katika masuala yote ya kidini na kisiasa jambo ambalo linaleta umoja kwa wananchi wake.
“Sisi tunafanya maridhiano na Amani katika nchi yetu, lakini wananchi hawawezi kuwa na Amani kama wanasumbuliwa na maradhi na zoezi hili la kuchangia damu halibagui dini wala Imani yoyote bali hii ni kama sadaka na ibada yenye maana Zaidi.”
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Taifa, Askofu Israel Maasa amemshukuru sana Mkuu huyo wa Mkoa kama mlezi wa Jumuiya hiyo Mkoani hapo kwa ushirikiano mkubwa anaoonyesha katika kuleta maridhiano ka kuhakikisha kuwa Amani inadumu kwenye Mkoa huo.
Ameongeza kuwa, Jumuiya hiyo imeridhia kuingia ubia na Serikali kuhakikisha kuwa masuala yote yahayohusiana na Amani yanaendana pia na maendeleo ya kijamii ambayo yanaambatana na wananchi kuwa na afya njema.
“Tunaamini hatuwezi kuridhiana katika masuala ya kuabudu kwasababu kila mtu ana Imani yake kutokana na misingi aliyowekewa, lakini inawezeka katika kuleta maendeleo ya jamii zetu ikiwemo kuelimishana juu ya masuala mbalimbali yanayogusa jamii zetu moja kwa moja.
Ikumbukwe kuwa, zoezi hili linafanyika kwa mara ya pili baada ya lile lililofanyika mwaka jana Jijini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kilele cha siku ya Maridhiano Kitaifa itakayofanyika Mkoani Mbeya Machi 6 mwaka huu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.