Na Elinipa Lupembe.
Mgeni rasmi na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella ameongoza harambee kupata fedha za kiasi cha shilingi milioni 90 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa majengo matatu kwenye kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Usharika wa Magungani ulioko kata ya Sokoni I Jiji la Arusha.
Akizungumza wakati wa kuongoza Harambee hiyo Mhe. Mongella ameushukuru uongozi wa kanisa kuwa kumualika kufanya kazi hiyo ya kumtumikia Mungu, ambayo amethibithisha na kuahidi kushirikiana nao,mpaka ujenzi huo utakapokamilika na usharika huo tarajali utakapozinduliwa na kuwa usharika kamili.
Amethibitisha kubarikiwa na kushibishwa na neno la Mungu lilohubiriwa lililowakumbusha waumini kujitoa na kuchangia kazi za Mungu na kuongeza kuwa yeye anaamini sadaka inayouma ndiyo sadaka ya kweli.
Aidha amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inatambu na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na madhehebu ya dini, kwa kutekeleza miradi mingi ya kuwahumiwa wananchi wa Tanzania, miradi ambayo kimsingi ingefanywa na serikali.
"Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anasisitiza viongozi wote wa serikali kushirikiana kwa karibu na makanisa na viongozi wa dini, kwa kuwa anathamini mchango unatolewa na Taasisi za dini kusadia jamii ya watanzania husani wenye kipato cha duni" Amesema Mhe. Mongella
Hata hivyo changizo hilo limefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi milioni 13,218,500, ikiwa fedha taslimu milioni 7.4 na ahadi shilingi milioni 5.7 huku milioni 67.7 zikihitajika kufikia mwendo wa milioni 90 uliopangwa.
Katika harambee hiyo Mkuu huyo wa mkoa kwa niaba ya ofisi yake amechangia kiasi shilingi milioni 5 kwa kutao fedha taslimu shilingi milioni 1 na kuahidi kukamilisha shilingi milioni 4 kabla ya tarehe ya uzinduzi wa usharika huo mapema mwezi Novemba 2023
Akiongoza ibaada, Mkuu wa Kanisa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Baba Askofu Dkt. Solomon Massagwa, kupitia neno la Mungu lililogusia suala la imani inayoendana na matendo, amewakumbusha waumini wa kanisa hilo katika harambee hiyo wakumbuke kumtolea Mungu sadaka iliyonona ili kukuza imani kwa wale waisoamini nao wamtukuze Mungu kupitia wao.
"Imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo, na imani inaendana na matendo imani isiyo na matendo, Biblia inasema imani hiyo imekufa, tunapomtolea Mungu leo, tunakamilisha imani zetu kama wakristo hivyo sadaka ya kumjengea Mungu kanisa inambariki Mungu na kuishi kwenye mioyo yetu" Amesema
Akisoma risala ya Harambee, Mchungaji Kiongozi Usharika Tarajali wa Magungani, Mch. Thomas Kaika amesema lengo la harambee hiyo ni kukusanya shilingi milioni 90 kwa ajili ya kukamilisha jengo la utawala, darasa la shule ya Jumapili pamoja na maliwato za kisasa kwa kuwa kitambo si kirefu usharika huo tarajali utakuwa Usharika Kamili.
"Tayari tulianza ujezi jengo limefikia hatua za kupandisha kuta na mpaka hapo tunahitaji milioni 90 fedha ambazo zitakamilisha ujenzi wa miundombinu pamoja na kuanda shughuli za usimikaji wa Usharika zinazotegemea kufanyika mwezi Novemba 2023" Ameweka wazi Kiongo wa Kanisa
Naye Mwenyekiti wa Changizo Mwl. Lidya Kikura , licha ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Mkuu wa mkoa wa Arusha kwa kukubali kushiriki kwenye harambee hiyo ya upanuzi wa miundombinu ya kanisa, amewashukuru pia washarika wote kwa kujitoa kwa hali na Mali bila kujali hali maisha, kipato na uchumi wao na kuwaomba kuendelea kuzoa Baraka hizo kwa Mungu kupitia matoleo yao.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Changizo Mwl. Lidya Kikura , licha ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Mkuu wa mkoa wa Arusha kwa kukubali kushiriki kwenye harambee hiyo ya upanuzi wa miundombinu ya kanisa, amewashukuru pia washarika wote kwa kujitoa kwa hali na Mali bila kujali hali maisha, kipato na uchumi wao na kuwaomba kuendelea kuzoa Baraka hizo kwa Mungu kupitia mayoleo yao
#arushafursalukuki
#KaziInaendelea
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.