Akizungumza na wananchi wa Kata ya Oldonyowas na Oldonyosambu Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amewataka wananchi hao kuacha mara moja tabia ya kuchoma shule ya sekondari Oldonyawas katika halmashauri ya Arusha.
RC Mongella amesema uchomaji wa shule hiyo umekuwa ukifanywa na watu wa eneo hilo mara kwa mra na wao wanawafahamu ila wanawaficha.
Amemtaka Diwani wa Kata ya Oldonyowas Kijana Saruni kuhakikisha uchomaji wa shule hiyo unaachwa mara moja kwani Serikali inaingia kwenye gharama kubwa ya ukarabati pasipo ulazima.
Sambamba na kusikiliza kero za wananchi RC Mongella amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri ya Arusha ikiwemo Elimu, Maji na Barabara.
Katika miradi hiyo, amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na kwa viwango vya ubora unaotakiwa.
RC Mongella amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Arusha ambapo alikagua miradi ya Elimu, Maji na Barabara na kusikiliza kero za wananchi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.