Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa ujenzi, wa shule mpya ya sekondari Engarnaibor, kata ya Mundarara wilaya ya Longido, mradi uliotekelezwa kwa ubora na kukamilika kwa wakati.
Mhe. Mongella ameonesha kuridhiahwa na hali ya utekelezaji wa mradi huo, mara baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo mpya, ambao tayari umekamilika ukiwa na viwango vya ubora unaokubalika kuendana na thamani ya fedha zilizotolewa na Serikali.
Amesema kuwa licha ya kata ya Mundarara kuwa umbali wa zaidi ya Km 30 kutoka makao makuu ya wilaya, kukiwa na gharama za usafirishaji na ufikishaji wa vifaa vya ujenzi eneo hilo, bado ujenzi umefanyika kwa viwango na kukamilika kwa wakati.
"Watumishi tukipewa dhamana ya kusimamia shughuli za maendeleo tujitoe, na kuwa waadilifu na wenye nidhamu na waaminifu kwa manufaa ya Umma, niwapongeze wasimamizi wa mradi huu, endeleeni na moyo huo ". Ameweka wazi Mhe. Mongella
Kaim Mkuu wa shule, sekondari Engarnaobor Mwl. Sabato Petro Nagagi, amesema kuwa, mradi huo umetekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 572, milioni 470 fedha kutoka serikali Kuu, kupitia mpango wa kuboresha miundo mbinu ya Elimu Sekodnari nchini (SEQUIP) na shilingi milioni 102 zikiwa ni fedha za mapato ya ndani ya halmashauri.
Ujenzi huo umejumuisha jengo la utawala, vyumba vya madarasa, maabara za masomo ya Sayansi, chumba cha TEHAMA, vyoo pamija na vyoo vya wanafunzi.
Awali mkuu wa mkoa wa Arusha, amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwilaya ya Longido, ikiwa ni maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mapema Januari 2023.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.