Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K.Mongella ameshiriki hafla ya uzinduzi wa Ubalozi Mdogo wa Uganda mkoani Arusha, eneo Uzunguni barabara ya Haile Sellasie, Jijini Arusha.
Akizungumza kwenye halfa hiyo, Mhe. Mongella ameishukuru Serikali ya Uganda, kwa kufungua ofisi ndogo za Ubalozi mkoani humo, kutokana na umuhimu wake wa uhusiano wa miaka mingi kati ya watu wa Arusha na watu wa Uganda na kukiri kuwa, Ofisi hizo zimechelewa kufunguliwa mkoani hapo.
Amethibitisha kuwa, upo uhusiano mkubwa na uliodumu kwa miongo mingi kati ya Tanzania na Uganda, hasa kwa kuzingatia Uganda ni miongoni mwa nchi za kwanza, kuungana na kuunda Jumuia ya Nchi za Afrika Mashariki na kuahidi kutoa ushirikiano wa kiseta wakati wote kama yalivyo maelekezo ya Serikali ya awamu ya sita.
"Serikali ya Tanzania, chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetuelekeza kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kwa nchi yoyote itakayofungua ofisi ndogo za balozi mkoani hapa, niwaahidi kudumisha ushirikiano baina yetu, zaidi niwakaribishe Arusha, ninaamini mtafurahia kuwepo Arusha" Ameweka wazi Mhe. Mongella.
Awali Ofisi ndogo za Ubalozi wa Uganda mkoani Arusha, imefunguliwa rasm na Naibu Waziri Mkuu, Jamhuri ya Uganda na Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Rebeca Kadaga, kwa kukata utepe leo tarehe 25 Novemba 2023, Barabara ya Haile Selassie na 20B, Jiji la Arusha.
HAILE SELASSIE ROAD NO.20B
ARUSHA MUNICIPALITY
P.O.BOX.2462
ARUSHA
#arushafursalukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.