• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

RC MONGELLA ASISITIZA  UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU, DAWA,  VIFAA NA VIFAA TIBA KWENYE VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA  AFYA...

Posted on: December 29th, 2023

Na Elinipa Lupembe

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella ametembelea na kukagua hali ya utoaji na upatikanaji wa huduma za afya, katika Kituo cha Afya Karatu, na kushuhudia wananchi wakiendelea kupata huduma za afya kama kawaida.

Akiwa kituoni hapo, Mkuu huyo wa mkoa, ameuagiza uongozi wa wilaya ya Karatu, kusimamia hali ya utunzaji na uhifadhi wa dawa, vifaa na vifaa tiba, huku akisistiza dawa ambazo hazijaanza kutumika, kuhamishiwa kwenye famasi kubwa ya hospitali ya Wilaya, hospitali ambayo inalo eneo maalum la kuhifadhia dawa, badala ya kuziacha kituoni hapo ambapo kuna eneo finyu.

Hata hivyo Mhe. Mongella ameendelea kukerwa na hali ya  utunzaji duni wa vifaa na miundombinu na kuwasisitiza watumishi wa Afya, kuwa wazalendo kwa kuthamini na kuvitunza vifaa vyote,  vinavyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na sio kuviacha viharibike ovyo.

"Wahudumu wa afya mnalo jukumu la kutunza vifaa na vifaa tiba katika maeneo yenu, ikiwa ni pamoja na kufanya ukarabati mdogo kwa vifaa vinavyohitaji matengenezo madogo madogo badala ya kusubiri viharibike kabisa na kusababisha Serikali kuingia gharama ya kununua upya, jambo ambalo linawezekana kuepukika.

Aidha, amesistiza kuharakisha kutengeneza generata la kituoni ambalo lilipata hitilafu, ili chumba cha kuhifadhia maiti kiendelee kufanya kazi, na kumtaka Mkurugenzi halmashauri ya Karatu kujipanga kukarabati jengo hilo la mochwari.

Hata hivyo, Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Karatu, Dkt. Iman Emmanuel, amesema kuwa,  generata la kituo liliharibika na kupelekwa kwa fundi,  tayari limeshatengenezwa na litarudishwa kituoni hapo kuendelea na kazi, huku akikiri kufanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa mkoa na kujipanga upya kurekebisha changamoto zilizooneka na kuendelea kutekeleza jukumu lao la kuwahudumia wagonjwa na kufikia malengo ya Serikali

Awali, Mhe. Mongella yupo wilayani Karatu kwa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa shughuli za  maendeleo kiskta za wilaya hiyo.

#aushafursalukuki

Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.