Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella aemkagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Longido, Mradi huo umetekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingi Bilioni 3.4, ambapo shilingi Bilioni 3 ni fedha kutoka Serikali Kuu huku shilingi milioni 340 ni fedha za mapambano dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO 19.
Hata hivyo Mhe. Mongella amemuagiza Mkuu wa wilaya hiyo kupitia halmashauri ya wialya ya Longido, kuchukua hatua za kubadilisha milango iliyowekwa kwenye majengo, milango ambayo inaonekana kutokuendana na hadhi ya mradi huo mkubwa unaotekelezwa na Serikali pamoja na kuingiza umeme wenye uwezo wa kuendesha mitambo iliyofungwa hospitalini hapo.
Aidha hospitali hiyo inategemea kuhudumia zaidi ya wagonjwa 175,915 wa wilaya ya Longido na wengine kutoka Nchi jirani ya Kenya, kukiwa na lengo la kutoa huduma zote za afya pamoja na kupungumza gharama kwa wagonjwa kusafiri mpaka Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru jijini Arusha, sambamba na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali hiyo ya Rufaa.
Kiasi hicho cha fedha Kimejumuisha ujenzi wa Jengo la Utawala, jengo la wagongwa wa nje OPD, jengo la Mionzi, jengo la wazazi, jengo la kufulia, jengo la dawa, wodi ya kina mama na wodi ya kinababa, maabara, jengo la kufulia na kichomea taka.
Hata hivyo fedha hizo zilikuja kwa awamu nne tofauti ambapo asilimia 100 ya majengo tayari yamejengwa huku majengo ,achache yakiwa kwenye hatua za mwisho zaa ukamilishaji.
Ikumbukwe kuwa ujenzi wa hospitali za wilaya chini ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM wa kuhakikisha kila Wilaya inakuwa na Hopitali kwa lengo la kusongeza huduma muhimu karibu na wananchi ikiwa na mpango maalum wa kupambana na kuzuia vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
#arushafursalukuki
#KaziInaendelea
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.