Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella amekutana na timu za Menejimenti za Halmashauri tano za mkoa huo, ikiwemo Jiji la Arusha, Monduli, Longido, Karatu na Ngorongoro kujadili Mapitio ya Rasimu ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025 za Halmashauri hizo, Kikao kilichofanyika kwwnyw ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa Arusha, Februari 06, 2024.
Kikao hicho kilichojadili masuala mbalimbali na mipango ya amendeleo ya Halmashauri hizo na mkoa wa Arusha kwa ujumla wake, wakati lengo kuu likiwa ni kupitia Mapendekezo ya Bajeti za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2024/2025, kupitia
maeneo ya vyanzo vya mapato na mikakati ya vyanzo vipya pamoja na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji mapato.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.