Na Elinipa Lupembe
Serikali ya awamu ya sita, kuelekea miaka mitatu ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, mkoa wa Arusha umekuwa miongoni mwa mikoa nchini, iliyonufaika sana kwa kupata miradi mingi ya maendeleo, inayokwenda sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Akizungumza wakati akitoa salamu za mkoa wa Arusha kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Hamad Mchengerwa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, amesema kuwa, Serikali ya awamu ya sita imetofa takribani trilioni 2 za kutekeleza miradi ya maendeleo, miradi ambayo imeleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii ikilinganishwa na awamu zilizotangulia.
Amesema kuwa, kiasi hicho cha fedha kinaweza kulinganishwa na fedha za miradi kwa miaka sita na kuongeza kuwa ipo miradi mikubwa ambayo haijawahi kutekelezwa katika mkoa huo, ikiwemo ujenzi wa shule mpya za sekondari na msingi, ujenzi wa vituo vipya vya afya na hospitali mpya za wilaya na mkoa, miradi ambayo inameshaanza kuleta matokeo makubwa sana kwa wananchi wa Arusha.
"Kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Arusha, tunaipongeza Serikali, kwa namna imeweza kuteleza Ilani ya CCM ya 2020 - 2025, tunampongeza na kuahidi kumuunga mkono, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi wa Arusha, tunaahidi kusimamia utekelezaji wa shughuli zote za maendeleo za mkoa wetu"
Amesisitiza kuwa, kwa kipindi cha wiki mbili mfululizo, mkoa unakwenda kupokea magari 9 leo, kwa ajili ya usimamizi wa shughuli za afya, jambo ambalo halijawahi kutokea zaidi linajidhihirisha wazi, Serikali ya mama Samia imedhamiria kuondoa kero za wananchi, kuwahudumia wagonjwa katika maeneo yao pamoja na kuondoa vifo vya mama na mtoto.
Hata hivyo,Mhe. Mchengerwa amewapongeza viongozi wa mkoa wa Arusha, kwa kazi nzuri ya usimamizi wa fedha na miradi ya maendeleo, inayotekelezwa katika mkoa huo, pamoja na ushirikiano mkubwa wa viongozi wa Chama na Serikali, ushirkiano unaosababisha hali ya amani na utulivu kwa wananchi wa mkoa huo.
"Ninawapongeza viongozi wote wa mkoa wa Arusha na Manyara, kwa ushirikiano wa karibu baina ya viongozi wa Chama na Serikali ni chachu ya mafanikio ya Serikali na wananchi, kila kiongozi wa aliyeteuliwa na kuchaguliwa anao wajibu wa kutekelza majukumu yake huku akitambua wote wanajenga nyumba moja" Amesema Mhe. Mchengerwa
Awali, Mhe. Mchengerwa, amekabidhi magari 13 yaliyotolewa na Serikali kwa ajili ya Usimamizi Shirikishi wa Shughuli za Afya kwenye mikoa ya Arusha na Manyara, huku Arusha ikipata magari 5 na Manyara magari 8, shughuli iliyofanyika leo tarehe 13.12.2023 kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.