Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, amewaongoza watumishi wa Serikali, Taasisi na Mashirika Umma na ya binafsi, wa mkoa wa Arusha, Kupanda miti eneo la Njiro, Ikiwa ni Kumbukizi ya Siku ya Kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani leo tarehe 27 Januari, 2024.
Katika Maadhimisho hayo, Mhe. Mongella amemuelezea Mhe. Rais kuwa ni Mpenda mazingira namba moja nchini, jambo ambalo lina wasukuma kusherehekea siku hiyo muhimu kwake kwa kupanda miti ili kutunza mazingira.
Ameweka wazikuwa, Mkoa wa Arusha umebarikiwa kuwa na maeneo ya Hifadhi, maeneo ambayo yanahitaji nguvu na juhudi kubwa kuyatunza, huku mkoa kwa kushirikiana na taasisi za Umma na binafsi kwa kushirikiana na mashirika ya Umma na yale yasiyo ya kiserikali kutunza na kuhifadhi maliasili hizo.
Ameweka wazi kuwa, Mlima Meru ni mlima muhimu kwa mkoa wa Arusha, kijamii na kiuchumi, huku mkoa huo ukiwekeza nguvu kubwa katika kuutunza kuanzia kwenye safu za mlima huo, ambazo baadhi yake zipo karibu na makazi ya Watu.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.