Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF), mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Hoteli ya Kimataifa ya Mount Meru Jijiji Arusha.
Mhe. Mongella ametumia wasaa huo kuwashukuru waandaji wa Mkutano huo kwa kuamua kufanyia mkutano huo Tanzania hususani katika mkoa wa Arusha.
"Kwa niaba ya Wananchi wa mkoa wa Arusha, tunawashukuru sana kwa kuupa heshima mkoa wetu kufanyika mkutano huu wa kimatifa, mkuatano ambao ni muhimu kwa wananchi wa Tanzania na Afrika" Amesema
Aidha amewakaribisha wageni na wajumbe wote wa mkutano kwa kuwahakikishia amani na usalama muda wote wawapo Arusha bila kusahahu hali nzuri ya hewa, hewa inayovutia kwa kila mtu anayefika Arusha.
Awali amewapongeza waandaji wa mkutano huo kwa kuweka ratiba ya kutembelea vivutio vya utalii vinavyopatikama Arusha, ikiwemo Mbuga ya Wanyama Ngorongoro na Olduvai Gorge, na kuweka wazi kuwa Olduvai Gorge ndipo lilipogundulika fuvu la binadamu wa kwanza, hivyo kama binadamu asili yetu ni Olduvai Gorge.
Hata hivyo Mhe. Mongella hakusita kuwashukuru wajumbe hao kwa programu ya kutembelea vivutio vya utalii ambavyo amekiri ni kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Filamu ya Royal Tour ya kutangaza Utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi, utalii ambao ndio msingi mama wa uchumi wa Tanzania.
#arushafursalukuki
#KaziIendelee
PICHA ZA MATUKIO
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.