Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella akizungumza na maelfu ya watu waliofika kwenye Mkutano wa neno la Mungu unaenda kwa jina la 'Washa Taa' unaoendeshwa na Taasisi ya Rise & Shine, na Mtumishi wa Mungu Mtume Boniface Godwin Mwamposa na kuthibitisha kuwa amani ya mkoa wa Arusha na nchi inachochewa na Watumishi wa Mungu.
Katika mkutano huo, Mhe. Mongella amepata wasaa wa kuwasalimia waumini walioshiriki mkutano huo na kumpongeza Mtume Mwambosa kwa kuandaa mkutano wa Neno la Mungu, mkutano ambao unawajenga wanaArusha kiimani na kuwafanya kudumisha amani, upendo na usalama wa mkoa wa Arusha na kuufanya mkoa kuwa na utulivu mkubwa.
Ameongeza kuwa serikali inatambua na kutahmini mchango wa viongozi wa dini na kwa kuwa serikali haima dini, kila mtanzania ana haki ya kuabudu imani yoyote huku utanzania ukiendela kuheshimiwa kupitia dini hizo.
Mutumishi ametulisha neno la kiroho, kwa neno linalotoa matumaini kwa wanaArusha, neno linalohimiza uadilifu, amani na nidhamu, kwa pamoja matendo haya ndio yanayosababisha amani na kuwasukuma wananchi kufanya kazi kwa maendeleo ya Taifa.
"Unapoona Arusha imetuliani ni kwa sababu watu wake wana amani na imani na nchi yao na serikali yao pia, inayotokana na neno la Mungu linaloendelea kutolewa na kuwajenga watu kuwa imara kiroho, nikuombe Mtume uje Arusha ikiwezekana hata mara tano kwa mwaka, matunda ya mikutano hii yanajidhihitisha wazi" Amesisitiza Mhe. Mongella.
Naye Mtume Mwambosa ameahidi kurudi mara kadhaa Arusha, hata kama haitafika mara tano lakini atakuja zaidi ya ratiba yao, kwa kuwa mkoa wa Arusha umejaa amani na utulivu huku ukiongozwa na Mkuu wa mkoa mwenye hofu ya Mungu.
"Serikali inapokuwa na viongozi wenye hofu ya Mungu ni baraka kwa Taifa, Mamlaka zote zimetoka kwa Mungu, viongozi watii kama Mkuu wa mkoa Mongella, huleta maendeleo katika nchi, na wananchi wake hufurahia baraka za Mungu wakati wote" Amesema Mtume Mwamposa
Katika mkutano huo wa Washa Taa, uliowakutanisha wakazi wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara, walipokea uponyaji wa miili na roho huku huduma ya kukanyaga mafuta ikifanyika.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.