Mkoa wa Arusha, unaadhimisha miaka 47 ya Chama cha Mapinduzi tangu kuzaliwa kwake mwaka 1977, ikiwa ni mwezi wa mwisho kukamilisha miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, imefanya mapinduzi ya maendeleo ya kiuchumi na Kijamii yaliyogusa sekta zote na hatimaye kumfikia mwananchi mmoja mmoja.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.John V.K Mongella, amethibitisha hayo, wakati akiwasilisha kishindo cha utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kupitia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika mko huo, kwenye maadhimisho ya miaka 48 tangu kuzaliwa Chama hicho, Februari 05, 1977, yaliyofanyika kimkoa, Mto wa Mbu, wilayani Monduli.
Amefafanua kuwa, kwa kipindi cha miaka mitatu, Serikali ya awamu ya sita, imefanya mapinduzi makubwa katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kuwasogezea karibu huduma za msingi katika maeneo yao huku duka hilo la Chama likisimamiwa vema na wauzaji ambao ni viongozi na watalamu wa fani mbalimbali mkoa wa Arusha.
Mhe. Mongella ameweka wazi kuwa Serikali ya awamu ya sita, imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 818.83 kwa ajili ya kutekeleza miradi kiseta, miradi ambayo hajawahi kutekelezwa kwa muda mfupi, tangu kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961.
"Sote tu mashahidi, katika maeneo yote kila kata na kijiji kimeguswa na fedha hizo, kwa idadi kubwa ya miradi iliyotekezwa kisekta kwenye maeneo wanaoishi wananchi hususani maeneo ya pembezoni, ameneo ya vijijini ambayo hapo awali yalionekana kutelekezwa" Amesema Mhe. Mongella.
Katika sekta ya elimu, mkoa wa Arusha umepokea shilingi bilioni 47.1 fedha zilitumika kujenga jumla ya shule mpya 16 za msingi na shule mpya 25 za sekondari katika wilaya zote za mkoa wa Arusha, huku wanafunzi wakisoma kwa uhuru na furaha kwenye mazingira rafiki, yasiyo na msongamano darasani.
Sekta ya afya nayo haikubaki nyuma, Serikali imetoa takribani Bilioni 32.8, fedha zilizojenga zahanati 45, vituo 18 vya afya, hospitali 7 pamoja na vifaa tiba na dawa, vituo ambavyo vimeongeza na kurahisisha utoaji na upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi huku dawa muhimu zikifikia 92%
Katika kuratibu na usimamizi wa utoaji wa huduma, Serikali imetoa magari 14 kwa ajili ya ufuatiliaji wa shughuli za afya, huku magari ya wagonjwa wa dharura 5 na lori la Kiliniki Jongezi (mobile clinick).
Kutokana na changamoto ya miundombinu ya barabara za ndani ya mkoa, Wakala wa Barabara TANROAD imeendelea kutengeneza barabara kwa kiwango cha lami, barabara za Ngorongoro Waso mpka Sale huku barabra ya Km 27 kutoka Mto wa Mbu mpaka Selela ikiwa kwenye hatua za awali za kuwekwa lami.
Nayo bajeti ya Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini - TARURA, imeongezeka kutoka Bilioni 19 na kufikia shilingi Bilioni 40, fedha ambazo zinaendelea kutengeneza na kukarabati barabara za ndani ya mkoa.
Katika kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya umeme, vijijini kupitia program ya REA jumla ya shilingi Bilioni 78 zimetolewa na huduma ya umeme imeshafikishwa kwenye vijiji 322 kati ya vijiji 329 ikiwa vimesalia vijiji 7 ambavyo kazi inaendelea na inategemea kukamilika mwezi Juni, huku mpango wa Taifa wa kufikisha ulele kwenye vitongoji ukiendlea kwa kasi.
Wakati huo huo, shirika la Umeme TANESCO mkoa wa Arusha, lileendelea kuimarisha na kuboresha miundombinu ya umeme kwenye maeneo ya viwanda na watumiaji wadogo, jumla ya shilingi Bilioni 21.1 zimetolewa na Serikali ya awamu ya sita.
Hali ya upatikanaji wa maji safi maeneo ya vijijini nayo imeendelea kuimarika, kupitia Mamlaka ya Maji Vijijini RUWASA, ikipokea shilingi Bilioni 28 huku miradi 63 ikitekelewza ndani ya halmashauti zote za mkoa wa Arusha.
Hata hivyo Serikali imeendelea kutoa fedha za kuhakikisha upatikanaji wa ma Maji Safi na Usafi wa Mazingira mijini, Mamlaka ya maji Arusha ( AUWSA) ikipatiwa shilingi bilioni 535, Bilioni 15 za kutekelza miradi midogo huku Bilioni 525 zikitekeleza mradi mkubwa wa Jiji la Arusha ambao unaelekea hatua za mwisho kukamilika.
Awali Mhe.Mongella amemshukuru Mhe. Rais kwa kuifungua Arusha, kupitia Filamu ya Royal Tour, Hali ya utalii imeimarika, kumekuwa na ongezeko kubwa la watalii, wanaotembelea vivutio vya utalii katika mkoa wa Arusha kwa kuunganisha misimu yote pamoja na uwepo wa Mikutano mikubwa ya kitaifa na kimataifa, ambayo imeleta amani kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na kujikita kupokea wageni, huku wakinufaika kwa kujipatia kipato na kupandisha pato la mkoa pia.
"Kipekee, nichukue fursa hii, kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Arusha, kuwashukuru viongozi wa CCM wa ngazi zote, kwa kushiriki kikamilifu kila mmoja kwa nafasi yake na kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali zinatumika kwa kusudi lililokusudia na kuwawezeha wananchi kupata huduma". Amesema Mhe.Mongella
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.