Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amembatana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justin Masejo kuwatembelea na kuwajulia hali Waandishi wa Habari waliolazwa katika Hospitali ya FAME -Karatu baada ya kujeruhiwa na Vijana wa Jamii ya Kimasai wakati wakitekeleza majukumu yao ya kikazi katika Kijiji cha Endulen Wilayani Ngorongoro.
Sambamba na hilo, Mongella ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kuwasaka na kuwakamata watu wote waliohusika na tukio hilo la kuwashambulia Waandishi hao wa Habari wakati wakiwa katika kutekeleza majukumu yao ya kikazi Wilayani Ngorongoro.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.