Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella amemuelezea, Hayati Edward Lowassa katika uhai wake, alikuwa ni kiongozi nguli wa maendeleo wa mkoa wa Arusha.
Mhe. Mongella ameyasema hayo wakati akitoa salamu za rambirambi, kwa niaba ya wananchi wa mkoa huo, kwenye ibaada ya mazishi ya Waziri Mkuu huyo Mstaafu, yaliyofanyika kijiji cha Ngarash, wilaya ya Monduli.
Amesema kuwa, wakati wote yanapozungumziwa maendeleo ya mkoa wa Arusha, huwezi acha kumtaja Hayati Lowassa, katika sekta zote za kijamii na kiuchumi huku akiweka wazi kuwa, kama mkoa wataendelea kuyaenzi mema yote aliyoyafanya katika mkoa wa Arusha.
Aidha, Mhe. Mongella amesema kuwa, wananchi wa mkoa wa Arusha wanamshukuru Mungu kwa maisha ya Hayati Lowassa, kwa kuwa aligusa maisha ya wana Atusha na amendeleo ya Arusha kieskta.
"Kwa niaba ya wananchi wa mkoa Arusha, tunatoa pope kwa familia mama na watoto na tutaendelea kushirikiana na familia huku tukiyaenzi maisha yake ya hapa duniani husussani katika utumishi wake wa Umma". Amebainisha Mhe. Mongella
Awali, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaongoza watanzania kwenye mazishi ya hayati Edward Lowassa, yaliyofanyika nyumbani kwake, kijiji cha Ngarash wilaya ya Monduli.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.