Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda amekutana na kundi la vijana linalo fahamika kwa jina la “Wadudu wa Arusha” nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kufanya mazungumzo mafupi na vijana hao mapema leo Aprili 27, 2024.
Katika mazungumzo hayo Mhe. Makonda ameahidi kuandaa tukio maalumu na Wadudu kabla ya sherehe za Mei Mosi ambayo zitafanyika kitaifa Mkoani Arusha kwa mwaka 2024, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi
Aidha, amewasihi Wadudu kuishi kwa upendo, akiwataka waandae mpango wa kutafuta pesa na kusisitiza kuwa yeye kama Mkuu wa Mkoa yupo tayari kufungua milango kwa Wadudu wa Arusha.
Awali, Mkuu wa Mkoa huyo, amewataka Wadudu kuhamasisha wakazi wa Mkoa wa Arusha kushiriki katika sherehe ya Mei Mosi na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Wadudu wamekubali kufanya hivyo mbele ya Mhe. Makonda
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.