"Mkoa wa Arusha tumepatiwa takribani Bilioni 20.7 kwa ajili ya Miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya Afya na elimu".
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella alipokuwa akifungua kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC), mapema leo hii, Jijini Arusha.
Mongella amesema katika fedha hizo Bilioni 2 ni fedha zilitokana na tozo za mitandao na bilioni 12.7 ni fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano ya UVIKO 19.
Alikadharika amesema, kwa sekta ya barabara TANROADS wamepokea kiasi cha Bilioni 13 na TARURA bajeti ya mwaka jana ilikuwa Bilioni 9 lakini mwaka huu Serikali ya awamu ya sita ikaongeza hadi kufikia Bilioni 19.
Jitihada zote hizo zinafanywa na Serikali ya awamu ya sita kwa lengo la kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma nzuri katika sekta zote iwe Afya, Elimu na watumie Barabara nzuri za viwango kwa shughuli za kujenga uchumi wao na Taifa kwa ujumla.
Pia, alisisitiza kwa vikao kama hivyo kujikita zaidi katika kuibua changamoto zinazowagusa zaidi wananchi moja kwa moja na kuzitafutia suluhu ili kujenga Mkoa wenye maendeleo zaidi.
Kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa ni kikao cha kwanza cha robo mwaka 2021/2022 kikiwa na lengo la kupitia mapato na matumizi ya bajeti kwa mwaka 2021/2022.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.