Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Silvia Mamkwe amewataka wanawake kujitokeza kupima kansa ya kizazi na wasiogipe kufaa kinachotumika kupima.
Ameyasema hayo alipokuwa akizunguza na waandishi wa habari katika semina ya wanahabari iliyofanyika Jijini Arusha.
"Amesema watu wengi wamekuwa wakikimbia kipimo hicho kwa kuhofia kifaa kinachotumika kuwa sio rafiki", alisema.
Dkt. Silvia amesisitiza kuwa kifaa kile ni rafiki na hakiumizi kama watu wanavyodhani.
Serikali imeamua kuwekeza zaidi katika chanjo na upimaji wa saratani ya kizazi kwasababu ni ugonjwa unaoleta vifo vingi kwa wanawake.
Amesisitiza kuwa, Saratani ya kizazi inatibika ikiwa mgonjwa amewai matibabu yake mapema.
Semina kwa wanahabari imefinyika chini ya Wizara ya Afya na ikiwa imejumuisha Mikao 4 ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.