Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, akimbeba mtoto wa mjasiriamali aliyekuwa kwenye Banda la Wajasiriamali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani, yaliyofanyika kwenye, viwanja vya Ngarenaro, Jijini Arusha na kuwasisitiza kina mama kutumia fursa ya madarasa ya awali yaliyojengwa na serikali, kuwapeleka watoto shule ili waendelee na shughuli za uzalishaji mali.
Katika kumkwamua Mwenamke na kuhakikisha watoto wote wanakwenda shule, Serikali ya awamu ya sita, imejenga vyumba vya kisasa vya madarasa ya awali, vinavyoruhusu watoto wa kuanzia miaka 4 kuandikishwa, na kuwasisyiza wanawake kuwapeleka watoto wa umri huo shule ili waendelee na kufanya shughuli zao za uzalishaji na kulijenga Taifa lao.
"Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, amejenga shule zenye madarasa ya Awali, zinazoruhusu watoto wa kuanzia miaka 4 kuandikishwa, jambo ambalo linamfanya mwanamke kuendelea kufanya shughuli za uzalishaji mali, huku akiwa amaemuacha mtoto kwenye mazingira na mikono salama ya mwalimu"Amesema Mkuu huyo wa wilaya.
Aidha, amewapongeza wanawake hao kwa kushiriki katika siku hiyo Maalum kwa wanawake wote Duniani, siku ambayo imeleta mwamko mkubwa kwa wanawake kwa kuwafanya kuwa wajasiri, kuungana kwa nguvu moja, kuinuana jambo ambalo limeleta mafanikio makubwa kwa wanawake wengi nchini.
Serikali imeendelea kusimamia sera za kuwakomboa na kuwainua wanawake kijamii na kiuchumi, kwa kuwajengea uwezo pamoja na kuwawezesha kuunda vikundi vya kuweka na kuwekeza na kuanziasha biashara ndogondogo na kupata mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa na Mamlakala za Serikali za Mitaa.
Kauli Mbiu ni "Wekeza kwa Mwanawake ili Kuharakisha Maendeleo ya Taifa Pamoja na Ustawi wa Jamii"
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.