Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainab Katimba amesema mwaka 2023/24, serikali inatarajia kuajiri walimu 12,000 wa masomo mbalimbali wakiwemo wa sayansi ambao watapangiwa vituo vya kazi katika maeneo yenye upungufu mkubwa ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.
Ameyasema hayo leo hii Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, wakati akijibu swali la Mhe.Minza Simon Mbunge wa viti maalum lililouliza, Je kuna mkakati gani wa kuongeza walimu wa sayansi katika shule za sekondari Wilaya ya Meatu.
Pia Mhe. Katimba amesema katika walimu 12,000 ambao wanatarajiwa kuajiriwa kwa mwaka huu kutazingatia na kuweka kipaombele wa upatikanaji wa walimu wa kike katika shule hizo.
“pamoja na kuwa serikali inaajiri walimu lakini hatua nyingine ambayo inachukuliwa na serikali ni kuhakikisha inafanya msawazo ili kupunguza walimu ambao wapo wengi kwenye shule nyingine kuwapunguza kwenye maeneo ambayo yanaupungufu mkubwa wa walimu” amesema Mhe. Katimba
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.