Naibu Waziri @ortamisemi anayeshughulikia Afya Mhe. Dkt. Festo Dugange (Mb) amesema Serikali inaendelea kutenga Fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya zahanati yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi, ambapo katika kipindi cha mwaka 2020/21 hadi 2022/23, Serikali imetoa jumla ya Shilingi Bilioni 89.9 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma 1,798 ya zahanati kote nchini.
Dkt.Dugange amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu wakati akijibu swali la Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina, Mbunge wa Jimbo la Kisesa aliyeuliza Je, ni lini Serikali itajenga Zahanati katika kila Kijiji Nchini ili kusogeza huduma ya afya kwa Wananchi.
“katika mwaka 2023/24 serikali imetenga shilingi bilioni 18.8 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma 376 ya zahanati kote nchini. Hadi kufikia machi, 2024 jumla ya shilingi bilioni 18.76 zimeshatolewa. Mpango wa serikali wa ujenzi wa zahanati katika vijiji ni endelevu. Serikali imeshafanya ukaguzi wa zahanati zote zilizojengwa kwa nguvu ya wananchi katika Halmashauri zote na imeendelea kutenga na Fedha kwaajili ya ukamilishaji wa maboma hayo” Mhe. Dugange.
Aidha katika hatua nyingine Mhe. Dkt. Dugange amemuelekeza Mkurugezi wa Halmashauli ya Nchemba kwa kushirikiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma kumpeleka Mtaalamu wa masuala ya Mionzi katika Hospitali ya Halmashauri ya Nchemba ili kuendelea kuwahudumia Wananchi.
Pia amesema serikali inaendela kuboresha Huduma za mionzi kwa kuwezesha kusimika machine za X – ray na ultrasound katika vituo vya kutolea huduma za afya msingi kote nchini ikiwa ni Pamoja na kuajiri wataalamu wa kutumia vifaa hivyo. Wakati akijibu Swali la nyongeza Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Nchemba Mhe. Mohamed Monni.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.