Na Elinipa Lupembe.
Kufuatia mkakati wa Serikali ya awamu ya sita ya kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu, kupitia program ya kuboresha miundombinu ya shule za Sekondari nchini (SEQUIP), mpango unaoenda sambamba na ujenzi wa nyumba za walimu, umewagusa na kukoga nyoyo za walimu kwa kuona Serikali inawajali.
Wakizungumza na mwandishi wetu, Walimu wa shule ya Sekondari Kiutu, halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha, wamethibitisha kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imekoga nyoyo za walimu nchini, kwa kuweka mazingira wezeshi wanayowapa unafuu katika tendo na kufundisha na kujifunza shuleni.
Wamesema kuwa tofauti na hapo awali, Serikali iliwekeza zaidi, katika kuimarisha miundombinu ya wanafunzi na kuwaachwa walimu, jambo ambalo liliwapa wakati mgumu katika ufundishaji lakini Serikali ya Awamu ya Sita imeenda mbali zaidi kwa kuwajali wanafunzi na walimu pia.
"Tendo la kujifunza na kufundisha linakwenda pamoja unapomuacha mmoja kati yao nyuma, inakuwa ni ngumu kufikia malengo ya uhamishaji wa maarifa kati ya mwalimu na mwanafunzi, unatengeneza uwazi 'gape',tunachelea kusema Serikali imetutendea haki walimu" Wamesema walimu hao
Mw. Fedrick Komba, amesema kuwa, shule ya sekondari Kiutu, ni shule mpya imejengwa majengo yote ya shule pamoja na nyumba ya walimu yenye sehemu za kuishi familia mbili, jambo ambalo wanaamini litaongeza tija katika ufundishaji na kupandisha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi..
Naye mwalimu wa Taaluma sekondari Kiutu, Mwl. Stanley Antony Mwampimbe, amesema kuwa kuwepo kwa nyumba nzuri za walimu zinawapunguzia makali ya maisha kwa kulipa kodi pale wanapoishi nyuma za kupanga, wanatumia gharama kubwa kulipa kodi za nyumba..
"Hapa Arusha gharama za maisha ziko juu na kusababisha kodi za nyumba kuwa juu pia, uwepo wa nyumba za walimu zinatupunguzia makali ya maisha, kwa serikali kutupunguzia mzigo wa kulipa kodi, walimu wa sasa tunaweza kuwa na maisha mazuri kama watumishi wengine wa Umma" Ameweka wazi Mwl. Mwampimbe.
Awali serikali kupitia mpango wa SEQUIP imejengea nyumba ya walimu yenye sehemu ya kuishi familia mbili (2in1), kwa shilingi milioni 98, shule ya sekondari Kiutu, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020 -2025.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.