Na Prisca Libaga Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora SMZ Haroun Ali Suleiman amesema jitihada za Wakuu wa Nchi SMT na SMZ na nia thabiti wanayoionyesha kwa vitendo katika kupambana na Rushwa ubadhirifu pamoja na ufisadi ambavyo vimekuwa sumu kubwa katika kurudisha nyuma maendeleo.
Aidha ametoa rai kwa Taasisi ya Wataalam wa Udhibiti udanganyifu wa Ubadhirifu ,Rushwa na uhujumu uchumi (ACFE) kushirikiana na sekretarieti za Mikoa na wilaya ili kudhibiti mianya ya rushwa katika miradi mbalimbali inatotekelezwa na serikali.
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la sita la chama cha wataalamu wa Udhibiti wa ufisadi ,Rushwa na ubadhirifu unaofanyika kwa siku tano Jijini Arusha na kuhudhuriwa na mamlaka mbalimbali za udhibiti wa Rushwa.
Alisema Rushwa na ubadhirifu bado ni tatizo kubwa ambalo halijadhibitiwa vya kutosha hivyo tuungane kwa pamoja kudhibiti suala hilo,licha ya viongozi wakuu kulipigia kelele, ingawa taaluma ya uchunguzi wa kubaini, (Certified fraud examiner CFE) vinaanisha kabla ya viashiria vya Rushwa kutokea kufanywa uchunguzi wa udhibiti.
"Kazi za ukaguzi katika udhibiti wa vitendo vya rushwa ufisadi na mapambano dhidi ya vitendo vya utakasishaji fedha haramu na namna bora ya kuimarisha utawala bora katika kudhibiti ufisadi serikalini na taasisi binafsi kwa upatikanaji wa ushahidi wa jinai na mada nyenginezo"
Kwa upande wake Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar CP Hamad Khamis Hamad amesema Kughushi nyaraka za miradi mbalimbali katika taasisi za serikali na binafsi ni mojawapo ya eneo ambalo halijapewa kipaumbele katika suala zina la mapambano ya ubadhirifu na uhujumu uchumi katika taasisi mbalimbali.
CP Hamad Alisema suala la wizi kwa kughushi nyaraka husababishia serikali hasa ambalo halijapewa umuhimu linapaswa kuangaliwa kwa jicho la kipekee badala ya kukamata mhalifu moja moja wa uhalifu wa kawaida ni wakati sasa kutumia ripoti ya mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG) ili kuwafikisha wahusika kwenye vyombo vya sheria.
"Ni wakati sasa kwa Wataalamu wa Mamlaka ya kuzuia Rushwa na uhujumu wa uchumi Zanzibar ZAECA,Takukuru Wakaguzi wa ndani serikali kwa kushirikiana na vyombo vya habari kuchambua taarifa ya CAG ili kubaini ubadhirifu unaotokea hasa katika kughushi maandishi unaopelekea serikali hasara katika usimamizi wa miradi ya serikali na taasisi za umma na binafsi"
Awali kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Rais wa Chama cha ACFE- T Ali Mabrouk Juma amesema serikali itambue taaluma ACFE kutumia kama bodi ya taaluma vyombo vinavyoshughulika na uchunguzi vikiwemo vyombo vya dola na Wakaguzi sanjari na taasisi ambazo zina miamala mikubwa kwa lengo la kubaini viashiria vya ufisadi.
Alisema moja ya changamoto sheria za Tanzania hazitoki nafasi nzuri kwa wataalamu wa uchunguzi walioidhinishwa kimataifa katika udhibiti wa ufisadi na ubadhirifu kama ilivyo katika sheria za nchi nyingine ambapo hutumika kama wataalam wanaokubalika inapotokea uadhirifu kama nchi ni vyema tukawa na watu waliothibitiwa kwa kupata vyeti.
Mada zitakazojadiliwa katika kongamano hilo la mwaka huu " mapambano dhidi ya rushwa ubadhirifu katika kutekeleza miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma za kijamii" rushwa na ubadhirifu ni tatizo kubwa lisilokadiriwa na halijadhibitiwa vya kutosha licha ya jitihada za dhati kulidhibiti.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.