Na Elinipa Lupembe
Kata ya Kamwanga ni miongoni mwa kata zilizopo mpakani mwa nchi ya Tanzania na Kenya, na mkoa wa Kilimanjaro wilaya za Siha na Rombo, takribani Kilomita 120 kutoka makao makuu ya wilaya.
Wananchi wa kata hiyo, wamewasilisha kero zao kwa serikali, mara baada ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. V.K.Mongella, kufanya mkutano wa hadhara na wananchi hao, ikiwa ni sehemu ya ratiba ya mkuu wa mkoa huyo akiwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo wilaya ya Longido.
Wananchi hao licha ya kushukuru ujio wa kiongozi wa wa mkoa, wamewasilisha changamoto zinazoikabili jamii hiyo na kukwamisha shughuli za maendeleo Kimwanga, na kuzitaja kero kuu ni pamoja na uhitaji wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Longido mpaka Kamwanga, ukamilishaji wa Kituo cha polisi, uwepo kituo cha afya pamoja na upatikanaji rahisi wa pembejeo za kilimo kwa kuwa shughuli kuu ya kiuchumi kwa wanachi hao ni kilimo.
Hata hivyo, Mhe. mongella ameweka wazi mkakati wa Serikali wa kuboresha miundombinu ya kutolea huduma kwa wananchi nchini, kadhalika inaendelea na mpango mkakati wa kuboresha miundombinu hiyo kisekta katika kata ya Kamwanga wilaya ya Longido.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.