Serikali imekabidhi magari 88 kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), magari ambayo yatasambazwa mikoa yote Tanzania, kwa lengo la kuongeza tija na kuboresha utendaji kazi wa Taasisi hiyo.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa @kassim_m_majaliwa, amekabidhi magari hayo kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan, wakati anafunga mafunzo ya awali ya uchunguzi ya Taasisi hiyo, hafla hiyo inafanyika kwenye Shule ya Polisi Tanzania, Moshi mkoani Kilimanjaro, Oktoba 26, 2024.
Mhe. Majaliwa ameitaka TAKUKURU kuongeza kasi na mikakati ya kudhibiti rushwa hasa katika maeneo ya ukusanyaji mapato, manunuzi wa umma, michakato ya ajira katika utumishi wa umma, mifumo ya ugawaji wa ardhi pamoja na utoaji wa huduma za jamii.
Akitoa taarifa ya magari hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila amemweleza kuwa, a katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani, TAKUKURU imepatiwa jumla ya Shilingi bilioni 30 za kununulia magari 195 ambapo 88 yameshanunuliwa.
“Mchakatio wa kununua magari 107 yaliyobakia unaendelea na tunatarajia kuyapata hivi karibuni, tunaahidi kutatunza magari haya ili kuongeza tija katika utendaji wetu” Amesema Bw. Crispin
Halfla hiyo pia imehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Boniface Simbachawene.
@takukuru.tz @owm_tz @kassim_m_majaliwa @ikulu_mawasiliano @msemajimkuuwaserikali
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.