• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

SERIKALI YAPATA MWAROBAINI WA KUONDOA  MAJUNGU NA UONEVU KWA WATUMISHI...

Posted on: December 17th, 2023

Na Daniel Gitaro


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora , Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema matumizi ya mfumo wa PIPMS, PEPMIS na HR Assessment katika Utumishi wa Umma nchini unaenda kuondoa tabia ya majungu na uonevu katika  Utumishi wa Umma huku akiwataka watumishi wa umma nchini kuupokea kwa mikono miwili mfumo huo.


Mhe. Kikwete ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru Mkoani Arusha,  ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Kupima Utendaji Kazi wa Watumishi wa Umma na Taasisi (PEPMIS na PIPMIS) na Mfumo Maalum wa Tathmini ya hali ya Rasilimali watu Serikalini (HR Assessment) yanayoendelea kufanyika mkoani humo.


Amesema mfumo wa OPRAS uligubikwa na udanganyifu, uonevu na upendeleo miongoni mwa watumishi, hivyo Serikali imekuja na mfumo wa kielektoniki ili kupunguza malalamiko ya watumishi wa Umma.


Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Kikwete amewataka Watumishi wa Umma nchini, kufurahia ujio wa mifumo hiyo mipya  kwani itatoa haki kwa wote na kuwafanya viongozi na watumishi wa Umma kwa ujumla kutekeleza majukumu yao kiuhalisia, tofauti na ilivyokuwa kwenye mfumo wa OPRAS.


Amefafanua kuwa  mfumo wa PEPMIS na PIPMIS ni mwarobaini wa masuala yote yaliyokuwa yakilalamikiwa na itasaidia kwa watumishi kupandishwa vyeo  kwa wakati.


Amesema kuna baadhi ya watumishi kazi yao kubwa wakifika maofisini, ni kuangalia nani kafika saa ngapi pamoja na kuchukua maneno huku na kupelekwa kwa wakuu wao ili mradi tu wapendwe.


Katika hatua nyingine, Mhe. Kikwete amesema mifumo hiyo mipya inakwenda kumlazimisha Mtumishi kutekeleza majukumu yake kwa fani aliyosomea na sio vinginevyo la sivyo mfumo huo utashindwa kumtambua.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru, Mwl. Zainab Makwinya amesema mifumo hiyo imekuja wakati muafaka kwani itatoa nafasi kwa watumishi kwenda kuwahudumia wananchi na sio kukaa maofisini.


Ameongeza kuwa  mfumo huo  utabaini watumishi wanaokwenda maofisini kusaini tu ili waonekane wapo na wale wanaokwenda ofisini kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.


#ArushaFursaLukuki

Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA 33 WA WAKUU WA MAJESHI YA ULINZI (SADC).

    May 30, 2025
  • SAMIA MOTOCROSS CHAMPIONSHIP KUREJEA MSIMU WA PILI JULAI 12, 2025

    May 27, 2025
  • MKOA WA ARUSHA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUBWA WA WAKUU WA MAJESHI WA SADC

    May 25, 2025
  • UJENZI WA UWANJA WA AFCON ARUSHA SIO MICHEZO TU, NI FURSA YA KIUCHUMI

    May 24, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.