SERIKALI YAPONGEZWA KUTENGA BILIONI 8 ZA KUPANGA ENEO LA UWANJA WA AFCON
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepongezwa kwa kutenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 8 kwaajili ya kuanza kutekeleza mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha (KKK) katika eneo lililopo pembezoni unapojengwa Uwanja wa mpira wa Afcon kata ya Olmoti Jiji la Arusha, mkoani Arusha.
Pongezi hizo zimetolewa na wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipotembelea eneo hilo, kujionea eneo unapotekelezwa mradi huo wa KKK pamoja na kujionea maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa Afcon, unaojengwa kwaajili ya mashindano ya mpira Afrika mwaka 2027.
Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Kamati hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Najma Murtaza Giga, amesema kuwa, tukio hilo ni la kihistoria ambapo Serikali imejipanga kukamilisha mradi wa ujenzi ndani ya miaka miwili na kuwataka wakandarasi kuongeze kasi ya upimaji wa maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kuanisha makazi na shughuli mbalimbalimbali za maendeleo zitakazofanyika kwenye eneo hilo.
"Arusha ina historia yake kwa utalii na fursa zingine hivyo tunahitaji taarifa kamili juu ya mradi huu ili tuweze kuishauri Serikali katika kuhakikisha vipaumbele vya awali vinapatikana na fursa za uwekezaji zinakuwepo kwani Afcon haipo mbali lazima tujipange". Amesema.
Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema fedha hizo zimetolewa na wizara hiyo kwaajili ya ulipaji wa ekari 207 za awali kati ya ekari zaidi ya 4,575.5 zilizopo katika mpango wote ambapo uwanja wa Afcon pekee una ekeri 83.
"Wizara imetenga fedha hizi kwa ajili ya kuanza ulipaji fidia na tunategemea tukimaliza kupima viwanja hivi tutanunua vingine hapo badae kadri wizara itakavyopata fedha kwaaajili ya kupima, kupanga na Kumilikisha lengo letu mji wa Arusha na maeneo mengine nchi nzima yapangwe". Amesema.
Mjumbe wa Kamati hiyo na mbunge wa Tabora, Mhe. Emmanuel Mwakasaka, amepongeza wizara hiyo kwa kuja na mkakati huo wa upimaji maeneo nchi nzima na kumshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa Uwanja huo wa Afcon.
@wizara_ya_ardhi @bunge.tanzania
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.