Serikali imesisitiza kuwekeza nguvu zaidi kwa watu walioathirika na urahibu wa dawa za kulevya, kwa kuwapatia huduma stahiki ikiwemo kuwarudisha katika maisha yao ya kawaida kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali sanjari na mikopo.
Rai hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Charles Mkombachepa kwa niaba ya akimuawakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda wakati wa Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga Dawa za kulevya Duniani Kanda ya kaskazini yaliyofanyika Jijini Arusha kwa ushirikiano na DCEA Kanda ya kaskazini na Kanisa la wasabato, yenye kauli mbiu; "wekeza kwenye Kinga na tiba dhidi ya dawa za kulevya".
Amesema kuwa, Serikali imewekeza katika elimu ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya hudusani kwa vijana pamoja na kuwahudumia waraibu hivyo ni vema kwenda mbele zaidi katika kuwajengea uwezo wa kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa elimu ya ujasiamali
hiyo inatoa ujumbe wa kutia nguvu kuikinga Jamii hususani vijana wasijihusishe na matumizi na uuzwaji wa dawa za kulevya pia wale wote waliothirika na matumizi warahibu tuwekeze kuwapatia matibabu ya urahibu wa dawa za kulevya na Elimu ya kuwarudisha katika Maisha.
Naye, Afisa Ustawi na Elimu DCEA Kanda kaskazini, Sarah Ndaba, amesema DCEA Kanda hiyo, itaendelea kuratibu shughuli za kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya katika Mikoa Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manyara, ikiwa ni pamoja na kuelimisha, kutoa huduma za ustawi wa jamii pamoja na operesheni dhidi ya wahalifu wote wa dawa za kulevya.
"Tumeamua kushirikiana na kanisa la Wasabato sababu upo uhusiano mkubwa kati ya watu kujihusisha na matumizi au biashara haramu ya dawa za kulevya na kukosa Imani ya Mungu na malezi ya kidini tunaamini madhehebu yote hayaruhusu waumini wao kujihusisha na dawa za kulevya hivyo, tukaamua kuunganisha nguvu, ikiwa dini zote zinapinga vita dawa za kulevya pia tumetoa Elimu kwa makundi ya watu 300,000 kuanzia juni 2023 hadi Juni 2024.
Akitoa ushuhuda Mmoja ya aliyekuwa muathirika wa dawa hizo Fredrick Remmy amesema zamani hatukuwa na Elimu ya dawa za kulevya ndio maana wengi wetu waliangamia
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.