Na Elinipa Lupembe.
Serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, imetimzia ahadi yake wka wananchi, kwa kuanza kutoa vitambulisho vya Taifa, maarufu kama NIDA, kwa wananchi waliojianzikiwasha nchini, mkoa wa Arusha ukiwa miongoni mwao, zoezi ambalo lilikwama kwa zaidi ya miaka minne sasa.
Akizungumza wakati wa akizindua zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya NIDA kimkoa, wilayani Karatu, Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K.Mongella, amesema kuwa, Serikali imekamilisha ahadi yake kwa wananchi waliojiandikisha kwa kuanza kuwagawia vitambulisho vyao vya taifa huku akiwahakikishia wakazi wa mkoa huo kuwa, kila mwananchi mwenye sifa atapata kitambulisho cha Taifa.
Amesema kuwa, takribani watu 931,221, waliojiandikisha mkoani hapo, watapata vitambulisho, na tayari vitambulisho 880,000 vimeshafika kwenye ofisi za NIDA wilaya zote za mkoa huo, tayari kugawanywa kwa wananchi.
Leo nimekabidhi vitambulisho 99,132 kwa Maafisa Watendaji wa kata za Wilaya ya Karatu, ili wakawakabidhi Watendaji wa vijiji na viwafikie wananchi kwenye maeneo yao.
Aidha amewaagiza Maafisa Watendaji, kuhakikisha vitambulisho hivyo vinagawiwa kwa walengwa ndani ya siku 14, na kwa waliofariki dunia vitambulisho visitolewe, bali virejeshwe Ofisi za NIDA za wilaya.
"Rai yangu kwa Watendaji wote, kila kitambulisho akabidhiwe mhusika mwenyewe, kusitokee ubabaishaji wowote, kwa mtu aliyefariki rudisheni taarifa zake NIDA, asikabidhiwe kitambulisho mtu asiyehusika"Ameweka wazi
Amesisitiza wananchi wenye sifa, kuona umuhimu wa kuwa na kitambulisho cha Taifa, kwa kuwa mwelekeo wa Serikali sasa, ni kuingiza taarifa za kila mtanzania kwenye mfumo wa kidijitali, ambao utarahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa kila mtanzania.
Hata hivyo wananchi wa Karatu wameishukuru Serikali, kupitia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa vitambulisho vyao, ambavyo wamekuwa wakivisubiri kwa muda mrefu huku wakipata usumbufu mkubwa, ikiwemo kukosa baadhi ya huduma zilizohitaji kuwa na kitambulisho hicho.
Bupe Alfred Mwankusye, mkazi na mjasiriamali wa Karatu mjini, ameweka wazi kuwa, licha ya kuishukuru Serikali kwa kuwakabidhi vitambulisho vyao na kuongeza kuwa, kutokuwa na vitambukisho vya NIDA, walikwama kwenye masuala ya mikopo kutoka Taasisi za fedha ambazo zililazimu kuwa na kitambulisho hicho
"Tunamshukuru mama Samia kwa kutupa vitambulisho, wananchi tuliteseka, hasa wajasiriamali tulipohitaji kuchukua mikopo ya kuendeleza biashara, kwa sasa mambo yetu yatakwenda kama tunavyopanga" Amesema Mwajabu Khasim,
"Tulipia changamoto nyingi, kuna wakati nilimpeleka mtoto shule, nikapata usumbufu sana kwa kutokuwa na kitambulisho cha NIDA kwa sasa tunasema Kazi iendelee". Martina Philipo.
Ikumbukwe kuwa, ugawaji wa vitambulisho vya Taifa kwa watanzania, ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ya mwaka 2020 - 2025
#ArushaFursaLukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.