• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Arusha Regional

The United Republic of Tanzania President Office Regional Administration and Local Government Arusha Regional

  • Home
  • About Us
    • History
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa mikoa waliopita-Arusha
    • Dira na dhima
    • The basics
    • Strategies
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Units
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • District
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Councils
    • Arusha CC
    • Arusha DC
    • Meru DC
    • Monduli DC
    • Karatu DC
    • Longido DC
    • Ngorongoro DC
  • Investment Opportunities
    • Tourism
    • Livestock
    • Agricultre
    • Industrial
  • Our Service
    • Health
    • Education
    • Water
    • Land
    • Tourism
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

SERIKALI YATOA MAGARI YA AFYA MKOA WA ARUSHA YENYE THAMANI YA MILIONI 646.3

Posted on: December 6th, 2023

Na Elinipa Lupembe 


Serikali ya awamu ya sita kupitia Ofis ya Rais TAMISEMI, imetoa magari manne ya kubeba wagonjwa na kutoa huduma za afya katika Halmashauri za wilaya ya Longido, Ngorongoro, Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru pamoja na lori moja kwaajili ya Kliniki tembezi yenye thamani ya sh. milioni 646.360 kwa mkoa wa Arusha.


Akikabidhi magari hayo kwa viongozi wa taasisi hizo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John V.K Mongella, amesisitiza kliniki hiyo tembezi ianzie wilayani Ngororongoro ili wananchi wapate huduma za afya katika maeneo yao kwa kadri ratiba itakavyopangwa.


Amesema, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, anafanya jitihada kubwa kuboresha sekta ya afya na ndio maana ametoa magari hayo, kwaajili ya kusaidia wananchi kupata huduma za afya karibu na maeneo yao na kuongeza kuwa magari hayo yaliyotolewa yanapaswa kutoa huduma za afya kwa wananchi na si vinginevyo.


"Serikali ya awamu ya sita ni Serikali ya vitendo magari haya ya kubeba wagonjwa yapo matatu na jiografia ya Mkoa wa Arusha kuna maeneo yana changamoto za ufikaji wake na utoaji huduma za afya ni changamoto hivyo nawashukuru wabunge wa Mkoa huu kwa kupitisha bajeti kadhaa zilizozaa matunda haya, naomba hii kliniki inayotembea itoe huduma kwa wananchi ikiwemo madaktari bingwa wawepo ili kutatua changamoto za wagonjwa katika maeneo husika"


Amesisitiza magari hayo yatunzwe chini ya Usimamizi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Charles Mkombachepa atakayepanga ratiba nzima ya mzunguko wa kliniki hiyo inayotembea kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo chanjo na huduma zinazohitajika kitaalamu.


Naye Mganga Mkuu wa  Mkoa wa Arusha, Dkt. Mkombachepa ameishukuru Serikali kwa kuboresha huduma za afya, ikiwemo utoaji wa magari hayo manne, ambayo yataenda kuokoa maisha ya wananchi ikiwemo wagonjwa wa dharura, wajawazito wanaojifungua na watoto wachanga wenye changamoto za kiafya.


Awali Mbunge wa Ngorongoro, Mhe. Emmanuel Ole Shangay ameshukuru kupata gari la wagonjwa (ambulance) na kliniki hiyo inayotembea ambazo zitaenda kuondoa changamoto za wananchi wa Ngororongoro ambao wanakaa mbali na vituo vya afya wale wa maeneo ya pembezoni.


"Tulikuwa tukipatiwa huduma za afya kwa kutumia ndege katika maeneo yasoyofikika lakini sasa hivi ndege hiyo imekuwa changamoto, gari la wagonjwa na hii Kliniki inayotembea itawezesha wananchi kupata huduma za afya kadri ratiba ilivyopangwa" Amefafanua Mbunge


Naye Mkuu wa Wilaya ya Longido, Marko Ng'umbi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwakumbuka wilaya hiyo na  kuwapatia gari la kubeba wagonjwa kwani wilaya hiyo ina zaidi vituo vya afya zaidi ya vitano lakini kutokana na  jiografia yake na mtawanyiko wa watu maeneo ya pembezoni ni changamoto na awali wilaya hiyo ilikuwa haina gari la wagonjwa.


Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ngorongoro, Lucas ole Seina amesema kuwa serikali kutoa magari hayo yataenda kuokoa maisha ya wananchi wenye changamoto za afya.


#ArushaFursaLukuki


Announcements

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • View All

Latest News

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
More Videos

Quick Links

  • Guildlines Towards the use of ICT In Government
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Public Servant Portal
  • Takwimu
  • TANAPA

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap
    • FAQ

Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.