Halmashauri za Mkoa wa Arusha zimetakiwa kutunga sheria ndogondogo zitakazo wataka wananchi wapande miti katika maeneo ya makazi yao ili kulinda uwoto wa asili ambao umeeza kutoweka.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Iddi Hassan Kimanta alipowaongoza wananchi wa wilaya ya Arumeru katika zoezi la upandaji Miti katika shule ya msingi Tuvaila kata ya Maji ya chai.
Amesema upandaji Miti ni muhimu kwa utunzaji wa Mazingira yetu na hasa kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha, Kimanta amesema maeneo yote yaliyopandwa Miti katika Mkoa wa Arusha atayafuatilia ili kuona kama miti hiyo ipo au haipo hivyo ni wajibu wa wenyeviti wa vijiji na mwenyeviti wa kamati za mazingira kusimamia.
Ikibainika maeneo hayo Miti haikuota basi viongozi hao watachukuliwa hatua.
Amesema Miti inafaida kubwa sana ikiwemo katika vyanja ya uchumi na utunzaji wa Mazingira.
Akitoa salamu za Wilaya hiyo kwa niaba ya wananchi, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro amesema, wilaya hiyo inaendelea kuenzi utamaduni wa kupanda Miti katika maeneo mbalimbali ilikutunza mazingira.
Amesema uongozi wa Wilaya umekuwa ukiwachukulia hatua kali wale wote wanavunja sheria za utunzaji Mazingira kwani kwa kufanya hivyo kumeweza kusaidia kupunguza ukataji wa Miti kiholela katika Wilaya hiyo.
Maadhimisho ya siku ya upandaji Miti, hufanyika kila mwaka Aprili Mosi na kwa mwaka huu maadhimisho hayo yamefanyika Kimkoa katika Wilaya ya Arumeru na jumla ya Miti 600,000 ilipandwa sambamba na kauli mbiu isemayo “Panda Miti kwa uhifadhi wa Mazingira, Maendeleo ya Viwanda na kuimarisha Uchumi”.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.