Shule ya Sekondari Kisimiri iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Mkoani Arusha imefanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha sita kwa kushika nafasi ya pili kitaifa kati ya shule 543 zilizofanya mtihani huo, huku shule ya Sekondari Kibaha ikishika nafasi ya kwanza na shule ya Sekondari Kemebos ikishika nafasi ya tatu,hii ni kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na baraza la mitihani Taifa.NY.pdf
Aidha matokeo haya ya shule ya Sekondari Kisimiri ni mwendelezo wa historia ya kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani hiyo ya kidato cha sita kwani kwa miaka 3 mfululizo imekuwa kwenye kundi la shule tatu bora kitaifa ,ambapo mwaka 2016 ilishika nafasi ya kwanza,mwaka 2017 ikashika nafasi ya tatu na kwa mwaka huu 2018 imeshika nafasi ya pili kitaifa kwa watahiniwa wake 67 kupata daraja la kwanza na la pili ikiwa 51 kati yao wamepata daraja la kwanza na 16 kupata daraja la pili.
Nuru ya shule hii ya Sekondari Kisimiri yazidi kuangaza kwenye Mkoa wa Arusha wenye shule 17 zenye watahiniwa zaidi ya 30 za Serikali na Binafsi 14.Shule zenye watahiniwa chini ya 30 kwa mkoa wa Arusha zipo 13 ikiwa shule 1 tuni ya serikali na 12 ni binafsi.
Ufahuru huu umepelekea Mkoa wa Arusha kupata shule nyingi zilizofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita,mbali na Kisimiri shule nyingine 10 zilizofanya vizuri zenye watahiniwa zaidi ya 30 ni;Iluboru,Embarway,Mlangarini,Gawako,Loliondo,Engutoto,Irikisongo,Maji ya chai,Nainokanoka.Shule iliyofanya vizuri yenye watahiniwa chini ya 30 ni Mwandet.
Hata hivyo baadhi ya shule katika Mkoa wa Arusha zinatakiwa kuongeza juhudi katika kuinua kiwango cha ufauru nazo ni; shule ya sekondari Florian na Makiba
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.