Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda Paul Makonda amebainisha kuwa kwa siku mbili za tangu kuanzia kwa kambi ya Matibabu kwenye Kliniki ya Madaktari Bingwa na Wabobezi mkoani humo tayari watu 6,434 wamehudumiwa na kupatiwa matibabu, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha
Akuzungumza na maelfu ya wananchi waliojitokeza kupatiwa huduma katika kambi hiyo ya madaktari Bingwa, Mhe. Makonda amesema kuwa, kwa siku mbili tayari wagonjwa 6,434 wameshahudumiwa na kupatiwa matibabu huku watu 25, wakipatiwa rufaa kwa matibabu ya ziada kwenye hospitali na Taasisi za Umma nchini.
Ametumia muda huo, kuwapongeza na kuwashukuru kambi ya Madaktari Bingwa na Wabobezi, wahuumu wote wa faya kwa kushurkiana na Ofisi yake kuwahudumia wagonjwa hao licha ya changamoto ya onhezeko lamidadi kubwa ya watu siku hadi siku lakini wameendelea kutoahuduma hadi usiku bila kuchoka wala kukata tamaa.
"Tunafahamu kazi ya madaktari sio rahisi sana, inahitaji moyo wa kipekee sana, niwapongeze watoa huduma wote, timu mzima ya usimamizi kwa kazi nzuri ambayo inarudisha matumiani yaliyopotea kwa wananchi wetu hasa wenye kipato duni, tuendelee kuchapa kazi, Arusha kwetu ni Afya na Kutafuta pesa" Amesema Mhe. Makonda.
Hata hivyo, ameweka wazi kuwa, kulingana na takwimu za siku hizo mbili zilizobainisha ongezeko la watu kwa kila siku hali inayowapa mwanga wa kusudio la kuongeza dawa zaidi pamoja na madaktari na wahudumuwa wa afya hadi kufikia 550.
"Kwa idadi hiyo ya watu tuliowahudumia kwa muda wa siku mbili inatoa picha halisi ya uhitaji, hali inayotulazimu kuongeza dawa ili kila anayefika hapa apate huduma, na nimeshamuagiza Mganga Mkuu kuongeza mabanda mengine na madaktari" Amesema
Kaulimbiu ya Kambi hii ya madaktari bingwa ni "Afya yako mtaji wako, kazi yetu ni kukupatia huduma bora"
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.