Wananchi wa Arusha wameendelea kuishukuru Serikali ya Mkoa wa Arusha chini ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda kutokana na Kambi ya madaktari bingwa inayoendelea kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid.
Wananchi hao wameonesha furaha yao kutokana na matibabu yanayoendelea kwenye Kambi hiyo ya matibabu, wakifurahishwa na uwepo wa Madaktari bingwa kutoka kwenye Hospitali na Taasisi za Matibabu zenye kuheshimika kitaifa na Kimataifa.
Aidha wananchi hao, mara zote wameendelea kumshukuru na kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Chistian Makonda @baba_keagan kwa ubunifu huo, uiloungwa mkono na wadau wa sekta ya afya nchini, na kuwezesha kambi hiyo kuweza kutoa huduma za vipimo, matibabu na dawa bila malipo kwa siku saba mfululizo
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.