Maafisa elimu na walimu wa Mkoa wa Arusha wameelekezwa kwenda kusisitiza somo la historia kwa wanafunzi wao ili waweze kujua walipotoka.
Yamesema hayo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jiji la Arusha katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania bara, Jijini Arusha.
" Hakuna kosa kubwa tutakalo lifanya la kushindwa kurithisha historia ya nchi yetu kwa vizazi vijavyo".
Hii itasababisha watoto wetu kutoona thamani ya amani, umoja na mshikamano ulioanzishwa na wahasisi wetu.
Aidha, amewashauri watu wanaposherekea miaka 60 ya Uhuru kila mmoja aweke malengo yatakayoacha alama kwa miaka 60 ijayo ili mkumbukwe.
Spika wa bunge la Afrika Mashariki Mhe. Mathias Ngoga amesema amani ya Tanzania imelifanya bara zima la Afrika kujivunia.
Hivyo amewataka watanzania kuilinda amani hiyo kwani kuna nchi zinatamani kuwa na amani kama hiyo.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Bi. Neema Omary ambae ni mzee aliyekuwemo kipindi cha kupata Uhuru wa Tanzania bara amesema muhasisi hayati mwalimu Nyerere alifanikiwa kuondoa matabaka baina ya Watanzania.
Kuna hatua kubwa ya maendeleo imefanywa ukilinganisha na enzi nchi inapata uhuru.
Musa Mkanga nae alikuwa miongoni mwa wazee waliokuwepo kipindi cha uhuru amesema baada ya uhuru usafiri uliokuwa unatumika ulikuwa ni treni na mabasi tu na safari kutoka Mkoa mmoja hadi mwingine ilikuwa inachukua siku 3 hadi 5 lakini sasa hivi njia za usafirishaji ni nyingi.
Hivyo amewahasa watanzania kuyaendeleza hayo mema yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Mkoa wa Arusha umeadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania bara kwa kufanya maonyesho ya wafanyabiashara pamoja na huduma ya kutoa chanjo ya UVIKO 19 kwa wananchi katika Viwanja Azimio la Arusha.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.