Wakuu wa shule zote za Sekondari Mkoani Arusha wametakiwa kuhakikisha wanatokomeza daraja la zero katika matokeo ya kidato cha nne kuanzia mwaka huu 2021.
Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Iddi Hassan Kimanta alipokuwa akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Arusha.
" Haiingii akilini mzazi anachangishwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa alafu mtoto wake anaishia kupata daraja la zero kidato cha nne", alisema Kimanta.
Kwa mkuu wa shule yeyote ambae shule yake itatoa daraja la zero atachukuliwa hatua kali,ikiwemo kuhamishwa kituo cha kazi.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.