Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Maulid amesema kuna umuhimu wa kuhakikisha wanawake na vijana wanaandaliwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye sekta ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo.
Kauli hiyo ameisema alipokuwa akifungua maonesho ya nanenane na sherehe za Wakulima na Wafugaji Kanda ya Kaskazini.
Amesema sekta ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji imekuwa na mchango mkubwa katika nchi.
Amesisitiza kuwa maonesho ya nanenane yatumike kuhakikisha teknolojia za Kilimo, Uvuvi na Ufugaji zinawafikia wananchi.
Lengo la maonesho ni kuongeza mnyororo wa thamani ili kuongeza zaidi fursa za upatikanaji wa chakula na kujenga uchumi wa mtu mmoja.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema zaidi ya asilimia 60 ya watanzania wapo kwenye sekta ya kilimo na uvuvi hivyo huchochea maendeleo.
Amesema maonesho hayo yamezidi kuimarika kila mwaka kwa kuleta tija kwa wananchi kwani wanapata elimu tofautitofauti kila mara.
Pia, maonesha haya yanaendelea kuleta chachu ya mabadilika katika sekta ya Kilimo,Uvuvi na Ufugaji.
Nae, Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga akizungumza kwaniaba ya wakuu wa Mikoa ya Manyara na Kilimanjaro amesema lengo la maonesho hayo nikutoa elimu kwa njia ya kuona na kubadilishana uzoefu kwa mikao hiyo 3.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya nanenane ambae pia ni Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Musa amesema maandalizi yalianza mwezi Aprili kwa kuandaa vitaru katika maeneno tofautitofauti.
Maonesho ya nanenane Kanda ya Kaskazini yamefunguliwa rasmi Agosti 3 yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo "Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mifumo ya chakula", na yanatarajiwa kufungwa Agosti 8.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.