Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amewaagiza wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha kuweka mikakati na kusimamia hali ya lishe na uwandikishaji wa bima ya Afya iliyoboreshwa (ICHF) katika maeneo yao.
Ameyasema hayo alipokuwa akiongoza kikao cha tathimini cha lishe na bima iliyoboreshwa Mkoa kwa mwaka 2020/2021.
Ametoa pongezi kwa wadau wote wa lishe kwa kuufanya Mkoa kushika nafasi ya pili Kitaifa mwaka 2019/2020 ikiongozwa na Mkoa wa Kigoma.
"Bado juhudi zinaitajika za kuboresha zaidi hali ya lishe hasa katika Halmashauri ambazo hazikufanya vizuri".
Kwa mwaka wa fedha 2021/2020 Halmashauri zimetenga kiasi cha shilingi Milioni 3.7 kama fedha za lishe kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 ambapo wastani wa Mkoa kwa kila mtoto ni shilingi 1,202.
Aidha, amesema swala la uwandikishaji wa bima ya Afya iliyoboreshwa nila umuhimu kwani Afya inabeba maisha ya watu hivyo viongozi wote walibebe kwa uzito zaidi.
Amesema viongozi wa kimala wanamchango mkubwa wa kuhakikisha elimu na hamasa zinawafikia wananchi,hivyo washirikishwe kikamilifu.
Kwa sasa hali ya uwandikishaji Kimkoa Hadi Juni 30, 2021 ni wanachama 19,581 na kati yao wanufaika ni 97,905 na kuufanya Mkoa kushika nafasi ya 12 Kitaifa kati ya Mikoa 26.
Nae, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Dkt.Athumani Kihamia ameshauri kuwepo na utaratibu wa uchangiaji wa fedha za lishe kwa Halmashauri zote kutoka katika chanzo kimoja ili kurahisisha katika ufanyaji tathimini.
Mkoa wa Arusha umejipanga katika kuhakikisha lishe na uwandikishaji wa bima ya Afya iliyoboreshwa zinafanya vizuri katika ngazi ya Kitaifa.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.