Nchi ya Sweden,kupitia Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha miradi ya maendeleo kwenye sekta ya elimu inakuwa kwa viwango vya ubora katika nchi zinazoendelea.
Kauli hiyo imetolewa na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe.Balozi Charlotta Ozaki Marcias, wakati akizungumza kwenye shule ya Msingi Muriet Darajani jijini Arusha leo Novemba 20, 2024.
Amesema kuwa, Serikali ya Sweden na Tanzania zitaendelea kushirikiana katika kusaidia sekta ya elimu nchini kupitia Ofisi y Rais,Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa lengo la kuhakikisha wanafunzi wanapata fursa ya kupata elimu kwenye mazingira bora na rafiki .
"Tumekuja kujionea fedha zinazotolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya elimu, miradi yake ipoje lakini tunafurahi kujionea uhalisia wa miradi ya shule zaidi tunaipongeza Serikali ya Tanzania kwa maendeleo yote wanayoyafanya katika sekta ya elimu"
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Dk,Charles Mahera aliishukuru Sweden na wadau wengine wa maendeleo kwa kusaidia sekta ya elimu ikiwemo madarasa,matundu ya vyoo,pamoja na miradi katika kuhakikikisha wanafunzi wasoma kwa bidii na kumshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya kuboresha sekta ya elimu
Ambapo Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa aliishukuru serikali na nchi ya Sweden kwakuhakikisha sekta ya elimu inakuwa zaidi na kuahidi kuisimamia kwa ukaribi miundombinu yote ya elimu na miradi inayotekekezwa ili kukuza kiwango Cha elimu nchini.
Awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Muriet Darajani,Dominic Gado amesema shule hiyo ni miongoni mwa shule zenye idadi kubwa ya wanafunzi ikiwa na jumla ya wanafunzi 5,263 huku bado ikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa miundombinu ya vyoo na madarasa.
Akizungumza kwa niaba ya Meya wa Jiji la Arusha, Diwani wa kata ya Ngarenaro Mhe. Isaya Doita ameweka wazi kuwa, Jiji la Arusha linaendelea kutenga fedha na kujenga kiundombinu ya madarasa na vyoo kwenye shule zenye idadi kubwa ya wanafunzi ili kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani.
Balozi Marcias aliambatana na mwakilishi wa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi wa Maendeleo kutoka nchini humo,Kemi Williams pamoja na Lucinda Ramos Alcanta ambaye ni Msimamizi wa GPE nchini na wadau wengine wa elimu, wamefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya elimu inayofadhiliwa na wadau wa maendeleo kupitia Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) kwaajili ya kukagua ujenzi wa shule ya awali ,vyoo katika shule ya msingi Muriet Darajani.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.