Taasisi ya CEDHA nchini Tanzania na Chuo Kikuu cha DMIHER nchini India wamesaini makubaliano ya ushirikiano kuboresha sekta ya afya nchini Tanzania na kuimarisha uwezo wa wafanyakazi wa afya, kukuza elimu ya madaktari bingwa, kufanya tafiti, sambamba na kutoa ushauri wa kitaalam.
Kupitia ushirikiano huu, Taasisi ya hizo zitatoa kozi fupi za utafiti, uongozi, utawala bora, na huduma kwa wateja kwa wafanyakazi wa afya Nchini.
Aidha, Madaktari bingwa kutoka Tanzania pia watapata fursa ya kujifunza katika vyuo vikuu bora nchini India.
Ushirikiano huu unalenga kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya afya nchini Tanzania sanjari na kuboresha huduma za afya kwa wananchi wote na kuimarisha mfumo wa afya kwa ujumla.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.