Na Elinipa Lupembe.
Nchi ya Tanzania imeendelea kuweka historia ya kidunia kwa mahusiano mazuri ya Kimataifa na nchi nyingi duniani, mahusiano yanayozingatia maslahi ya kichumi, kijamii na mwendelezo wa Sera za ndani za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella, wakati akifungua rasmi Kongamano la kukusanya Maoni ya wadau kuhusu marekebisho ya Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001, kongamano lililofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) Jijini Arusha leo 13 Novemba, 2023.
Amesema kuwa, Sera ya Mambo ya Nje iliyopita ya mwaka 2001 imeleta mafanikio makubwa kwenye Nchi ya Tanznania, ikiwa ni pamoja na kudumisha mahusino mazuri na Nchi jirani, ukanda wa SADC na Kimataifa, kupitia misingi iliyowekwa na waasisi wa Taifa hilo, hivyo ni vyema wadau hao kuichukulia kwa uzito unaostahil,i kwa msitakabali wa Nchi ya Tanzania kwa Miongo kadhaa mbele.
“Kutokana na unyeti wa Ajenda hii, washiriki wote kwa nafasi zenu mnalo jukumu la kuelewa mawasilisho yote hatua kwa hatua, ili kupata uwezo wa kuchangia kikamilifu mawazo, ambayo yatachakatwa mpaka ngazi ya Taifa, tumieni nafasi hii adhimu kwa manufaa ya Taifa letu”Ameweka wazi Mhe. Mongella
Hata hivyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Justine Kisoka, amesema kuwa, licha ya mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Sera iliyopita, bado kunahitajika maboresho zaidi ili kukuza uhusino wa Kimataifa.
“Yapo mambo mapya ya kujumuishwa kwenye Sera hii, ili tuweze kunufaika zaidi kama Nchi, ikiwemo uchumi wa bluu ambao ni kipaumbele kwa nchi yetu ya Tanzania, pamoja na ushirikishwa wa watanzania waishio nje ya Nchi na raia wote wenye asili ya Tanzania waishio nchi nyingine ili waweze kujumuishwa katika kuchangia maendeleo ya Taifa lao”. Amesema Kisoka
Kwa upande wake Afisa wa Ofisi ya Rais Zanzibar, Salum Mohamed Ramia, amesema kuwa maoboresho ya Sera hiyo, ni kwa manufaa ya Watanzania wote, ikiwa imesheheni maeneo mengine mapya yenye kuleta tija huku Sera ya Uchumi wa bluu, ikiwa ni moja ya kipengele kitakachopewa kipaumbele.
Ikumbukwe kuwa, Sera hiyo ilitungwa mwaka 2001 na mchakato wake wa utekelezaji kuanza mwaka 2004 sasa inafanyiwa uboreshaji kwa kupokea maoni kutoka kwa wadau wa Sekta mbalimbali za binafsi na Umma.
#mahusianoyakimataifa
#uchumiwabluu
#arushafursalukuki
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.