Na Elinipa Lupembe
Mawakala wa makampuni 102 ya Utalii kutoka nchini Marekani wamewasili mkoani Arusha kwa ushirikiano wa Bodi ya Utalii (TTBL) na Kampuni ya Excelent Tour Guide kampuni ya kizalendo ya Marekeni, kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujadili namna ya kuunganisha fursa katika sekta ya Utalii kati ya Marekani na Tanzania
Wakiwa nchini Mawakala hao wamekutana na wadau wengine wa utalii pamoja na mambo mengine ya kikazi, watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini ikiwemo Arusha na Zanzibar na kufanya mkutano na wadau wanutalii.
Wakizungumza wakati wa hafla ya Chakula cha Jioni, 'Dinner Galla' kwenye hoteli ya Mount Meru wamesema kuwa, wako Tanzania kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa namna ya kuwaleta watalii zaidi kutoka nchini Marekani kufuatia matangazo ya vivutio vya utalii vya Tanzania kupitia Filamu ya Royal Tour.
Mshirika wa Kampuni la Excellent Tour Guide, kampuni ya Kitalii ya kizalendo nchini Marekani, Lynn McCormick amesema kuwa, Mawakala hao wanaounganisha watalii wa Kimarekani kuja Tanzania, wamefanya mpango wa kuanzisha safari za moja kwa moja za ndege kutoka Marekani mpaka Tanzania ili kupunguza gharama na usumbufu kwa watalii watakaokuja Tanzania.
"Kukiwa na 'route' ya moja kwa moja kutoka Marekani mpaka Tanzania, itawapa fursa watalii wengi zaidi kutoka Marekani na kutembelea Tanzania" Amesema Lynn
Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii (TTB), Damas Mfugale amesema kuwa ujio wa mawakala hao utaongeza fursa ya watalii wa kimarekani nchi ambayo inaleta watalii wengi kufika Tanzania na kutembelea vivuti vya utalii kupitia pango wao wa kuanzisha safari za ndego za moja kwa moja kutoka nchini Marekani na kutua Tanznania, mpango ambao ni fursa ya kiuchumi kwa Tanzania.
Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella amesema kuwa, ujio wa Mawakala hao wa utalii utaongeza idadi ya watalii kutoka nchi ya Marekani, na kufikia lengo la watalii elfu tano kwa mwaka, jambo ambalo litachangia kwa kiasi kikubwa pato la Taifa.
Amesema kuwa serikali imejipanga na kuwekeza fedha kwenye miundombinu ya viwanja vya ndege nchini huku vianjwa vya mkoa wa Arusha, vikifanyiwa ukarabati mkubwa ili kurahisihsa safari za ndani za watalii, na kuongeza kuwa asilimia 80 ya watalii wanatokea Marekani, hivyo kupitia mawakala hao, kunategemewa kuwa na ongezeko kubwa la watalii nchini hususani mkoa wa Arusha.
"Tunazidi kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassani, haya ni matunda ya Filamu Ya Royal Tour, tunaona namna gani hata raia wa nchi nyingine wanaunga mkono juhudi hizi za serikali yetu ya awamu ya sita, kama mkoa na wananchi wote Arusha, tumejipanga vema kuwapokea na kuwapa huduma stahiki watalii watakaofika mkoani Arusha" Amesisitiza Mhel Mongella
Awali Filamu ya Royal Tour iliyochezwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ilizinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani, ikiwa na lengo la kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana nchini Tanzania jambo ambalo limegungua milango kwa watalii wengi kufika nchini hususani mkoani Arusha kwa ajili ya kutazama vivuti hivyo.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.